Lakini kama tena unamatumaini ya kuishi tambua kwamba unagharama ya kulipa kwani maisha ynabebwa na tumaini au njozi. Sasa kwa hali yoyote ile kama unanjozi au matumaini tambua kwamba unagharama ya kulipa. Gharama ninayoizungumzia hapa si gharama ya pesa tu bali na katika maeneo mengine ya maisha. Zifuatazo ni gharama ambazo unapaswa kulipia ili kuliendea tumaini lako.
Utayari. Utayari ni moja ya gharama ambayo unapaswa kulipia ili kuliendea tumaini lako. Kama una ndoto harafu unaishia kutaka tu hutapata kile ambacho unakitaka. Ni lazima uamini na uwe tayari kubadilika. Hii ni gharama ambayo unapaswa kulipa kwani hapa kama umepata tumaini na ulikuwa unaishi mazoea ya jambo fulani ni lazima uvunje misingi ya mwanzo na uweke misingi mipya. Sasa inakutegemea misingi ya mwanzoni uliiweka kwa muda gani na gharama gani.
Wakati. Wakati ni gharama pia ambayo unapaswa kulipia. Mungu huwa anatufunza kwa viwango tofautitofauti sasa hapa ni lazima uvumilivu ufanye kazi hapa. Sio siku moja utaamuka na kuifikia jambo unalotaka ama hata kama tumaini lako ni dogo lazima wakati upo ambao unapaswa kuchukua hatua fulani.
Mahusiano. Hii ni gharama ambayo inahusishwa na watu tofautitofauti. Wakati mwingine wale watu wa karibu kabisa lazima uwaache katika hali ya mshangao fulani. Wakati mwingine watu hawata kuelewa bali wewe unaelewa unachokifanya. Wakati mwingine unahitaji kulipa gharama ili kuwa na watu sahihi ambao unahitaji kwenda nao sambamba, Yote hii ni gharama katika mahusiano.
Kujifunza. Lazima ulipe gharama ya kujifunza kwani wakati mwingine unapaswa kulipia maarifa na taarifa mbalimbali. Hapa napo utalipia gharama ya muda wa kujifunza.
Zipo gharama nyingine ambazo utalipia wakati unaendelea kuliendea tumaini lako lakini hizi ni moja kati ya gharama ambazo unapaswa kulipa wakati unaliendea tumaini lako.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment