Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima. Karibu tena katika Falsafa Za Maisha.
Kuna maana nyingi sana katika neno Falsafa. Kuna watu wanaitwa Wana Falsafa, watu ambao waliishi maisha yao hapo nyuma. Na wengine bado wana njia zao hata sasa za kuishi na wanaita Falsafa.
Lakini mwisho wa yote, Falsafa maana yake ni pendo la hekima, yaani neno la maarifa katika maisha.
Sasa, tutakuwa tukishirikiana kwa ufupi, katika mwendelezo ule kwa kadili Mungu atakavyotujalia, tutakuwa tukivunja makufuli katika neno la Mungu kwa kadili ambavyo Mungu atatujalia.
Kwa njia hii, tutakuwa tunafunuliwa mafunuo ya neno la Mungu.
Kwa leo, tujue Falsafa inaanzia wapi katika muundo wake, maana twasema Falsafa ni neno la maarifa, ama, Pendo la hekima.
Falsafa inaanzia pale, mtu anapoanza kujenga picha katika ubongo wake, kutoka katika akili hisia.
Naam, ni maarifa katika mkazo wa kwanza na mwendelezo wa mikazo hiyo.
Kwa leo tunaishia hapa.
KIMA, MWANA WA KIMA.
PENDO LA HEKIMA.
Sadick Lazaro Kilasi.
0687000768
0 comments:
Post a Comment