Katika mazingira tunayoishi tunaweza kuanza na kidogo ambacho Mungu ametubariki na tukafanya makubwa tu ambayo yatakuwa baraka kwa watu wengine. Kila mtu anakitu cha kuanzia, akivaa utayari wa kufanya hilo jambo ni wazi kwamba atafika mbali sana.
Warumi 10:17, Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Kwa dhana hii au mfumo huu, kwamba, unaamini kitu na kwa kadili ambavyo unaamini ndivyo utataka kujua zaidi. Kwa hiyo kaa na utambue kwamba siku zote ulichonacho hata kama ni kidogo kiasi gani, unaweza kukikuuza na kuwa kibwa sana. Hivyo, tumepewa mwanzo ambao unaweza kutupeleka mbali zaidi.
Jambo la kujiuliza ni hili, ni eneo gani unahitaji kukua zaidi na kujitanua zaidi, ni wewe tu, kuwekeza kwako muda mwingi ndiko kunaweza kukufanya ukue zaidi. Chagua mambo ambayo yatakujenga na ukue kwa hayo. Asante.
Nisadie kusambaza hizi makala ili ziweze kuwafikia wengi zaidi.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment