Nilinunua kitabu changu cha kwanza, muuzaji akanishawishi nichukue kitabu cha BWANA WETU ALIYEFANYIKA KUWA HAKI YA MUNGU. Kitabu hiki kilikuwa ni kikubwa, sasa katika fikira zangu nilikuwa nawaza kwamba mwandishi aliyekuwa ameandika kitabu hicho alikuwa na itikadi kali za kidini. Niliwaza tu moyoni kwamba watu wanaoandika mavitabu makubwa haya ya kidini ni lazima tu wanavutia kwao. Lakini muuzaji akaniambia chukua mimi nitakupunguzia bei. Nikachukua kitabu.
Nilisoma kwanza kitabu kingine nikawa nimemaliza baada ya siku tatu. Nikaanza kusoma kile kitabu cha BWANA WETU ALIYEFANYIKA KUWA HAKI YA MUNGU. Kwa mara ya kwanza ndipo nilikutana na injili ya maji na Roho. Mwandishi wa kitabu hiki Paulo C Jong alikuwa anajaribu kuchambua vizuri kabisa kitabu cha Warumi. Nilijikuta sasa naona badala ya kuishia kutazama tu. Nilimwelewa na ndipo nilipojijua mimi ni nani mbele za Mungu. Nikawa najaribu kulinganishia kwenye Biblia nikaona. Siku hiyo nilitafakari sana, nakumbuka niliandika makala, juu ya mambo niliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki, harafu nikasema nimevunja misingi yote ambayo nilijifunza utotoni ya kidini na naanza upya, na sijui ujasiri huo niliupata wapi.
SOMA:Mambo Niliyojifunza Kutoka Kwenye Kitabu Cha BWANA WETU ALIYEFANYIKA KUWA HAKI YA MUNGU (II).
Nilikuwa sijafanikiwa kumpokea Roho Mtakatifu, japo sijui,neno linasema, Marko 4:26-29, Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi; akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika. Kwa sababu Yesu ndiye anayebatiza mimi sijua kitu gani kinaendelea, lakini niliiamini injili hii ya MAJI NA ROHO.
Kwa sababu kwenye kitabu kile alikuwa ameonyesha vitabu vyake ambavyo ameandika, nilikona kitabu chenye jina la NJIA YA TAHADHARI YA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU, nikasema, sasa hiki kitabu nakihitaji, nikampigia simu muuza vitabu akaniambia, hicho kitabu hakipo ila ataenda kuangalia anakochukulia, baada ya siku tatu hivi akanipigia simu jioni, nikaenda Posta, nikavkuta vitabu vyake vitatu pamoja na hivyo nikachukua vyote pamoja na hicho nilichokuwa nahitaji. Nikaanza kusoma kile kitabu na kwa namna ambavyo alikuwa ananionyesha injili ya maji na Roho ilivo nilielewa vizuri. Mungu akasema, chukua mundu yako kavune mavuno uliyopanda. Tangu siku hiyo, maisha yalibadilika ghafla, siku moja tu, niliingia dunia ya furaha. Mpaka sasa nadumu katika neno la Mungu na kwa kadili ninavosoma Biblia ndivyo napata haki ya Mungu zaidi.
Ninamshukuru Mungu kwa kumtoa Mwanaye Yesu Kristo ili achukue dhambi zangu. Sina dhambi kwa sababu Yesu alichukua dhambi zangu. Alipobatizwa na Yohana pale Yordani ndipo sasa mizigo yangu ilichukuliwa, na sasa nipo huru.
Lakini kwako wewe rafiki yangu, hii ni bahati yako au ni wakati sahihi kwako? Mimi sijui chukua hatua, siku moja tu hubadili historia ya maisha ya mtu. Kitabu cha UKRISTO NA MAISHA ni kitabu ambacho nimeielezea injili hii ya maji na Roho na unapoiamini injili hii unapokea haki ya Mungu. Jipatie kitabu hiki bure kabisa, hiki ndio kitu ambacho naweza kukupa haijarishi upo katika hali gani? Wewe ni maskini au tajiri.
Sadick Kilasi wa jikolaushuri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment