Warren.
Upo kwa jinsi ulivyo kwa sababu Umngu alikuandaa uwe kwa jinsi ulivyo. Mshukuru Mungu kwa kukupa upekee ambao haufanani na mtu yeyote.
Tupo hapa duniani kwa sababu Mungu aliandaa dunia iwe sehemu yetu sisi kupitia kama maisha baada ya kupewa miili yetu. Mshukuru Mungu kwa hilo kwa sababu ukiwa na mwili umekuwa mkamirifu.
Una sura hiyo uliyonayo kwa sababu ya wazazi wako waliunganika kwa upendo na wakakufanya uwe wewe. Waheshimu wazazi wako na uwape shukrani.
Mtu fulani amekaa kivulini leo kwa sababu mtu fulani alipanda mti miaka ya nyuma.
Mpendwa msomaji, panda mti, panda mti ambao watu watakuja kukaa na kupata kivuli ambacho watajivunia kwa sababu ya wewe.
Fanya kitu ambacho dunia itaendelea kukumbuka hata kama haupo licha ya kwamba hutakumbukwa milele lakini angalau uishi miaka zaidi ya miaka uliyoishi.
Wewe ni barua iliyotumwa na Mungu, ni lazima upande mti ambao Mungu alikutaka uupande ili uje ulete kivuli ulimwenguni. Hakuma mtu aliyezaliwa bahati mbaya, kila mtu alizaliwa kwa kusudi lake, kama Mitume walizaliwa kuhubiri injili basi Mtume Paulo alizaliwa kusambaza injili kwa mataifa. Kila mtu amepewa kitengo cha kuendeleza pale ambapo mwenzie kafikia.
Kama upo kwenye mti uliopandwa na mtu fulani wa mwanzo basi na wewe ongeza mti mmoja zaidi ili kuonyesha kwa umekubali kilichoanzishwa na wa kale.
Panda mti leo uje ukusaidie baadae wewe mwenyewe na kizazi kijacho.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

0 comments:
Post a Comment