JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Sunday, September 30, 2018

Toa Ulichonacho, Anzia Hapo Ulipo.

 Sadick Kilasi     September 30, 2018     TAFAKARI YA ROHO     No comments   


KANUNI YA KUTOA KAFARA.

Kafara ama kwa lugha nyingine sadaka ni kitu ambacho unatumia ili kuhusianisha kati yako wewe na kitu ambacho unataka kukipata. Ikiwa mtu hajatoa kafara katika jambo analotaka kulifanya basi ni ngumu kulifanya hilo jambo. Mara nyingi huwa baada ya kupokea jambo fulani jipya ambalo tumelipenda na tungehitaji kulipata huwa tunakwepa gharama ya maumivu ya mwanzo. Ukweli ni kwamba kilajambo ambalo ni sahihi na ni kweli huwa linahitaji kulipa gharama fulani mwanzo mwa hilo jambo. Na mara nyingi gharama ile ndiyo inakuwa ukuta mkubwa sana wa kufikia jambo hilo ambalo mtu anapaswa kulichukulia hatua. Japo kuwa licha ya kuwepo gharama ya kulipa mwanzo sio kwamba lile jambo huwa haliwezekani bali mhusika huwa anakwepa kijanja kulifanya jambo lile. Zipo sababu ambazo mara nyingi humzuia mtu kutokufanya jambo ambalo anataka kulifanya. Mazoea huwa yanafanya mtu asichukue hatua fulani. Ikiwa mtu una uraibu wa kufanya jambo fulani, kuachana na jambo hilo na kuanza kufanya jambo jipya inakuwa ni ngumu sana. Ni pale sasa ambapo unahitaji kujitoa mzima mzima, kujitoa wewe mwenyewe kama kafara.

Sababu nyingine ni vijisababu visivyoeleweka huweza kusababisha kutofanya jambo jipya. Unaweza ukawa unatamani kufanya jambo fulani lakini unaweka sababu ambazo hazilingani kabisa na kusudi lako, lakini wakati mwingine sababu hizo zikawa zinaleta maana kabisa kwako wewe binafsi na kwa wengine pia wanaokusikiliza.

Biblia huonyesha namna ya kujitoa katika hali fulani ya mazoea ambayo mtu amezoea kufanya.
Mahubiri ya Yohana. Mathayo 3:1-10.
Siku zilealiondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribi. Kwa sababu huyo ndiye aliye nenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, itengenezeni njia ya Bwana, yangyosheni mapito yake. Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi, wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; naye akawabatiza katika mto Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya nyinyi kukimbia hasira itakayokuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba; wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawambia ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. Na shoka limeshawekwa kwenye mashina ya miti; basi kila mti usioweza kuzaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

Ubatizo maana yake kuzamia katika jambo fulani,zamisha kwenye maji. Ikiwa mtu amekiri toba, kuna madhehebu mengine huwabatiza watu kwa kuwazamisha kwenye maji kama ishara ya kusafisha dhambi. Lakini lengo kubwa kuwazamisha katika maji bali lengo kubwa ni kufanya yanayofaa kufanywa. Ikiwa kweli umetubu basi utaonyesha kwa matendo na ndio maana Yohana aliwaka hasira kwa Mafarisayo na Masadukayo, sio kuamini tu bali wanapaswa kuonyesha kwa matendo kulingana na imani yao.

Luka 3:10-14,Makutano wakamwuliza, tufanye nini basi? Akawajibu akawambia, mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo. Watoza ushurunao wakaja kubatizwa, wakamwuliza Mwalimu, tufanye nini sisi? Akawambia, msitoze kitu zaidi kuliko ulivoamriwa. Askarri nao wakamwuliza sisi tufanye nini? akawambia, msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu.

Ikiwa mtu unasumbuliwa na jambo fulani ambalo limekuwa uraibu kwako na linakufanya ukose furaha na unashindwa namna ya kujitoa kilicho muhimu ni kutubu, kwa kukiri kwamba sasa nipo hapa na natubu kwa kuacha kufanya jambo jingine jipya. Kuna uraibu wa mambo mbalimbali, kubishana, kulala sana, mawazo mengi,kuangalia tivi sana, kujikuta unapenda kwenda mahali fulani bila sababu na tabia nyingine ambazo umezoeza na baadae ikawa usumbufu kwako. Kumbuka rafiki yangu, ninachofanya hapa ni kuhubiri injili kwahiyo, umakini wako ndio utakufanya uponywe kutoka na hali mbalimbali. Wakati Yohana alipokuwa akihubiri injili, akitokea jangwani, injili ya wito wa toba, watu walikuwa wamejizoeza kuabudu sanamu, wamejawa na dhambi na mambo mengine machafu. Lakini Yohana alikuja kugeuza mioyo yao, kwa kuwambia tubuni, yaani geuka, na kuonyesha matunda baada ya kugeuka kwamba umeamini kile unachokigeukia unafanya kwa matendo. Yohana alikuwa anageza mioyo ya watu ambao walikuwa wanaenda kuangamia kwa kkufanya mambo yasiyo faa, wito wake ni kugeuza mioyo yao na kuwambia wachukue  hatua za  matunda ya imani mpya.

Unaweza kijikuta upo katika hali ya maumivu wakati mwingine, kutokana na tabia ambayo umeiendekeza kwani mwili hukulazimisha ufanye jambo ambalo wewe mwenyewe hutaki; Warumi 7:19, Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Katika hali kama hii unaweza kujikuta katika wakati mgumu sana, kwa sababu kuna vita inakuwa inaendlea ndani yako.  Katika hali hii unahitaji kutimiza mapenzi yako kwa kile ambacho unadhamilia kufanya, kwa uwezo ulionao mwenyewe. Usiishie kusema nataka kufanya jambo fulani, hapana. inakupasa imani yako uunganishe na matendo yako. Usione kama huwezi kuchukua hatua yoyote, kwani kiashilia cha maumivu hayo, kinaonyesha kwamba unapaswa kufanya jambo ambalo ni sahihi.
2Wakorintho 8:11, Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza kwa kadiri mlivyo navyo. Kutokana na utayari wako unahitaji kutimiza mapenzi ya Mungu kutokana na utayari wa Moyo wako. Unaanzia pale ulipo kujitoa wewe mwenyewe, kwani hatupo sawa. Unaweza kuangalia pembeni wakati unajitoa ufanya jambo fulani, au unaweza kuangali mtu mwingine wakati unafanya jambo fulani, waweza kujikuta lile jambo hulifanyi kwa sababu unaweza kujiona kana kwamba huna pa kuanzia ama hujakamirika. Ukweli ni kwamba , tunahitaji kukamirisha kile ambacho tunacho na si kile ambacho wengine wanacho.

Ni lazima sisi wenyewe tujitoe katika kufanya jambo lililo sahihi, ikiwa unahisi kwamba hujakamirika basi ukijitoa mzima mzima kwenye jambo hilo basi utakuwa umekamirika. 2Wakorintho 8:1-3, Tena ndugu zetu, twaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongzea utajri wa ukalimu wao. Maana wanashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiyari yao wenyewe walitoa vitu vyao. Pale ambapo unahisi kana kwamba huwezi kutoa kitu, hapo ndipo unajionyesha unaweza kutoa kitu, maana mtu hawezi kuzungumzia kitu ambacho hakipo. Anzia pale ulipo na ujitoe kafara katika hilo unalotaka kufanya.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ▼  September (43)
      • Toa Ulichonacho, Anzia Hapo Ulipo.
      • Panda Mti Leo.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..13] Hatupokei Haki Ya Mungu...
      • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.
      • Usijikinai Ndugu, Utaoza.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..12] Injili Ya Maji Na ROHO....
      • Utukufu Ni Wa Mungu.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..11] Je! Ufanye Nini Wakati ...
      • Watu Hawatakosa La Kusema, Endelea Kufanya Unachop...
      • [TAFAKARI NENO YA LEO...10] Hamna Namna, Mshangaze...
      • Endelea Kufanya Yanayofaa.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO...9] Ukimpokea Yesu Onyesha...
      • Hii ndio Njaa Kubwa Ya Dunia Ya Sasa.
      • Tumia Makombo Ya Wakati Wako Kujisomea Neno La Mungu.
      • Naomba Uniambie Rafiki Yangu, Unaishije Na Watu Wa...
      • Una Shina La Kukupeleka Katika Ushindi.
      • Je! Mungu Atakuwepo Au Hatakuwepo?
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..8] Mambo Mawili Ambayo Huon...
      • Ukiona Unaliamini Jambo Na Huishi Hilo Jambo Basi ...
      • Je! Unapanda, Au Unashuka Bondeni?
      • Huwezi Kuuona Umuhimu Wa Maji Mpaka Visima Vikauke.
      • Kuijua Imani Na Kuishi Maisha Ya Ushindi.
      • Ukiona Fursa Hazigongi Mlango Jenga Mlango.
      • Jenga Tabia Hii Nayo Tabia Itakujenga Katika Mahus...
      • Gharama Ya KupataVitu Vizuri Vinavyokupeleka Katik...
      • [TAFAKALI NENO YA LEO...7] Ondoleo La Hofu Na Mais...
      • [TAFAKARI HEKIMA ZA WAZEE], Kuwaelewa Wengine, Kuj...
      • Alituchagua Tangu Tukiwa Na Dhambi. [Kwa Imani Tun...
      • Kanuni Ya Kibiblia Ambayo Inaweza Kukusaidia Kupan...
      • Utabiri Wa Nabii Danieli Juu Ya Injili Ya Maji Na ...
      • [TAFAKARI NENO YA LEO...6] Tumeandaliwa Mazingira ...
      • Umezaliwa Wa Kipekee Sana Lakini Watu Ndio Kioo Ch...
      • (TAFAKARI NENO YA LEO...5) Kama Una Tumaini Basi T...
      • Hakuna Mtu ambaye Hana Kabisa Katika Maisha.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..4] Mtumainie Mungu Usikate ...
      • Hii Ni Bahati Yako Au Ni Wakati Sahihi Kwako?
      • [TAFAKARI NENO YA LEO 3] Usiende Kwa Mganga Siku Y...
      • Tunapokea Na Kutoa Kutokana Na Utayari Tulionao....2
      • [TAFAKARI NENO YA LEO...2] Je! Unataka Kuwa Na Fur...
      • Geuza Machungu Yako Kuwa Ushindi.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO ...1] Jinsi Chuki Zinavyoene...
      • Tafakari Neno Ya Siku.
      • Tunapokea Na Kutoa Kwa Utayari Tulionao.
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates