Lakini pia huwa naamini kwamba sio kila jambo ni kweli wakati wote kuna wakati jambo hilo linawezakuwa kweli na kunawakati mwingine sio kweli. Sio kweli kwamba lazima kila mtu awe tajiri mkubwa lakini pia sio kweli kwamba si lazima mtu awe maskini. Ukweli wenyewe halisia ni pale mtu unapoishi ndani ya wakati kwa wakati sahihi.
Ukitaka uone umuhimu wa maji basi kosa maji. Sio usahihi wa ukweli kwamba anayeiba ni mwizi bali anayemtangazia mwenziye mwizi basi yeye ndiye mwizi namba moja.
Si kila neno ambalo unamtolea mtu kutoka kwenye kinywa chako huwa anasikiliza bali wakati mwingine mwingine maneno mengine unaweza kuongea yakarudi kwako kupitia sikio lako yakaumiza moyo wako. Kwa hiyo jiangalie na maneno yako.
Sio kweli kwamba unapaswa kuwa na ndoto wakati wote bali unapaswa kuishi ndoto kwani ndoto huwezi kuifikia na ukiifikia umekufa. Ishi sasa.
Ukweli ni kwamba, anayekwambia kitu na kukwambia uweke siri, usite kumwambia kwamba mizigo yake huwezi kujitwisha. Siri ni mzigo mzito sana ambao wakati wote unatamani kuutua. Wezi hutamani siri ya wanachokiiba, wanamafanikio hutamani siri ya Mafanikio na ndio maana sehemu za siri hutafutwa kwa uchu sana na watu japo ni sehemu za aibu.
Usitumie muda wako kumdanganya mtu kwa hiyo itakuwa ni siri yako.
Huwezi kuona umuhimu mpaka visima vikauke kwani huwezi kujua kudondoka mpaka uteleze.
Usimhukumu anayeiba wewe siumeweka siri na siri siku zote hufumbuliwa.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment