Kwa hili huwa namshukuru Mungu, naona kama ni upendeleo fulani ambao Mungu kanipa kwa sababu kwa mapito yangu ninaelewa hapa nilipo nipo wapi na nipo katika hatua gani. Kuna watu ambao hawawezi kuangalia mapito yao ya nyuma na kuyageuza kuwa ushindi kwao. Hili huwa linanifanya nielewa kwamba wapo watu ambao wapo hivo ni pale ambapo ninakumbuka miaka miwili nyuma ambapo nilikuwa sijaelewa kabisa kuhusu maisha yangu. Lakini leo naangalia nyuma na kumpa Mungu shukrani kwa yale ambayo nimepitia. Kuna mengine niliyatazama kwa jicho la ubaya na mengine niliyatazma kwa jicho la wema. Lakini yote kwa yote ilikuwa nikufanya mimi niyaelewe mambo na sasa yote ni mema kwangu.
Leo hii ninaweza kumsamehe mtu akinukosea, leo hii naweza kuelewa ni namna gani ambavyo watu huwa wanajisikia wakikosewa na hii inanifanya niwaombe msamaha haraka. Lakini yote haya ni Mungu, yeye ambaye huandaa majira kwa wakati wake. Ninaelewa namna gani ambavyo kwanini napaswa kuomba msamaha na pia naelewa namna gani namna watu huwa wanajisikia wakiombwa msamaha. Na hata kama watu wakaelewa tofauti na mimi ninavoelewa na kuwachukulia bado huwa najielewa kwamba mimi si mkamirifu sana sasa hapo ndipo huwa nageuza machungu yangu kuwa ushindi. Na hata kama nikifanya kosa, ninamshukuru Mungu ambaye ameniwekea upumgufu kidogo ambao ndio nguvu yangu ya kusimama tena.
Unaweza kufikiri namna gani Mungu kakuumba kwa ajabu. Unaweza kufikiri namna gani Mungu katuandalia mazingira tunayoishi yawe msaada kwetu kwaajiri ya kujifunza. Unaweza kufikiri namna gani vitabu vitakatifu vimeandaliawa kwaajili yako wewe uishi vema. Unaweza kufikiri namna gani watu wengi walitolewa kufa na wengine walifanyika watu wabaya ili wewe uwasome na uishi vizuri. Unaweza kufikiri kwa kumwangalia sisimizi tu, mdudu mdogo namna anavofanya kazi na wewe ukamwiga na kuishi maisha yenye maana. Fikiri hivyo rafiki yangu na umpe shukrani Mungu aliyekuumba. Angalia kwa mfano watu waliofamikiwa, walimwangalia ndege mnyama na kutengeneza ndege ya kupanda watu. Tumepewa kila kitu ambacho tuweza kugeuza kuwa ushindi kwetu. Hizi zote ni hekima za Mungu lakini yote ni kwaajiri yetu tujifunze ili tuishi maisha ya ushindi. USITUMIE VIBAYA ULICHOBARIKIWA NA MUNGU.
Mungu anaacha tupitie katika hali fulani ili tutazame na tuone namna gani baadae tuwe wakamirifu katika hilo. Kugeuza uchungu kuwa kuwa ushindi ni pale unapoona wema kwenye kila, ni pale ambapo unakuwa na shukrani.
Nguvu ya mtu ni furaha na msingi wa furaha ni amani na amani mwanzo wake kumcha Mungu, maana yeye ndiye Mfalme wa amani na kumcha Mungu huanza kwa shukrani. Maana Makuhani zamani walikuwa wanaingia patakatifu huku wakiwa na chetezo na kuvukizia uvumba. Rafiki, Ndugu yangu, chagua shukrani na ugeuze machungu yako kuwa ushindi.
Kama bado hujabahatika kusoma kitabu cha UKRISTO NA MAISHA, basi tafadhari unapaswa kukisoma kitabu hiki. Pia ombi langu rafiki yangu, unisaidie kusambaza makala hii na kazi zangu kwa ujumla ili watu wengi wapate kuponywa. Kazi hizi haziwezi kufika mbali zaidi bila wewe rafiki yangu, naomba msaada wako.
Sadick Kilasi wa jikolaushhauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment