Changamoto kubwa tulionayo kwa sasa ni kwamba kila mtu anataka tu yeye, watu wote wapo upande mmoja. Hayupo mtu ambaye yupo tayari kuchukua madhaifu ya mwingine. Kila mtu atakwambia nampenda anayenipennda. Rafiki yangu, hii inaleta maana, kila mtu anataka kupendwa tu, sasa nani atampenda mwenzie? Leo hii hata mwanzo wa ndoa, watu wanajaribiana kwanza tabia, je hii inaleta maana? Je, chanya kwa chanya zinaweza kujifiti kwa pamoja. Mwanaume alitolewa ubavu wake ili autafute ubavu wake, mwanamke anapaswa kufitisha lile pengo na mwisho wawe mwili mmoja. Mpendwa msomaji, upendo wa kweli ni kupenda kisicho pendeka.
Mwanzo 2:21-24, Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito,naye akalala, kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akamfanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema sasa huyu ni mifipa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi, ataitwa mwanamke kwa sababu ametwaliwa katika mwanamme. Kwa hiyo mwanamme na mwanamke atamwacha baba na mama yake, naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Rafiki, sizungumzii upendo wa mke na mme tu, nazungumzia upendo wote kwa ujumla. Kamilisha upendo penda pale palipokosa upendo.
Mpendwa msomaji, njaa kubwa ya watu hivi sasa, kufarijiana. Watu wanahitaji kufarijiwa lakini ni nani atakaye wafariji, ni nani atakaye amsha mioyo iliyovunjika? Kila mtu anahitaji kufarijiwa, usimwangalie mtu kwa nje tu, watu wamekosa hamasa katika maisha yao. Wanahitaji neno kutoka kwako wewe rafiki yangu, neno la matumaini. Haihitaji gharama kusema neno, haihitaji gharama kumsifiamtuambaye amekufanyia mambo mazuri, hata kama ni kidogo kiasi gani. Kiimani mambo madogo ndio makubwa sana. Anza kujari mambo madogomadogo ambayo watu wanakufanyia, utabadilika wewe binafsi hata wengine pia itakuwa njema kwao.
Tumia maneno kama asante, hongera, kazi yako ni nzuri, umependeza na mengine mengi kutokana na mazingira ambayo upo. Tena zidisha zaidi kwa adui zako. Weka mpango hivi sasa, wafariji watu angalau wawili kila siku, kwa maneno tu. Chagua wale watu ambao hamuendani ili ukamirishe faraja.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment