Lao Tzu
Ni ngumu sana kuwaelewa wengine kama wewe mwenyewe hujajielewa na ni ngumu sana kuwahimili wengine kama wewe mwenyewe huwezi kujihimili. Kwa ili kuwaelewa wengine anza wewe kujielewa, na ili kuwahimili wengine anza wewe mwenyewe kujihimili.
Katika ukuaji wa utu hizi ni hatua mbili muhimu sana. Hatua ya kwanza kujielewa na hatua ya pili ni kujihimili mwenyewe. Ni rahisi kumwelewa mwingine kama wewe mwenyewe unajielewa na ni rahisi kuhiimili mwingine kama wewe mwenyewe unajihimili.
Katika hayo yanabebwa na amri kuu mbili za Mungu, Marko 12:29-31, Yesu akajibu, ya kwanza ndiyo hii: Sakiliza Israeli! Bwana Mungu wetu ndiye peke yake BWANA, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii: Mpende jilani yako kama unavojipenda mwenyewe. Hakuna amri iliyo kubwa zaidi kuliko hizi.
Ili kujielewa ili uwaelewe wengine, hakikisha unampenda Mungu kwa kusoma mazingira ambayo Mungu kakuandalia, kujisomea vitabu bila kusahau kusoma neno la Mungu na hicho ndicho kioo cha kujiona wewe mwenywe. Ukisha kujielewa kupitia neno lake takatifu na kujifunza kutoka kwa watu watu, ni rahisi kuwaelewa wengine. Hapo ndipo utatimiza amri zote mbili ya kumpenda Mungu na kumpenda jilani yako kama unavojipenda mwenyewe.
Ili uweze kujihimili wewe mwenyewe, anza kuwa mwadirifu kwa kile unachojifunza kutoka kwenye neno la Mungu Hakikisha unachojifunza unachukua hatua na kufanyia kazi. Kwa kadili ambavyo unakuwa na nidhamu na uadirifu katika yale unayojifunza ndivyo unaweza kuwahimili wengine.
Chukua hatua: Jielewe, jihimili, waelewe, wahimili.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com..
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.

0 comments:
Post a Comment