JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Saturday, September 22, 2018

Je! Unapanda, Au Unashuka Bondeni?

 Sadick Kilasi     September 22, 2018     KUFURAHIA MAISHA, TAFAKARI YA ROHO     No comments   

Je! Unapanda Au Unashuka Bondeni?


Katika maisha hakuna kubaki sehemu moja kama hupandi ama hushuki. Kwa sababu ya dunia jinsi ilivyo, dunia ambayo imetawaliwa na nguvu hasi kabisa. Kama huna unachokifanya ambacho kinakupeleka mbele basi tambua dunia inakushusha chini. Huwezi kubaki palepale.

Ikiwa utapanda mbegu mbovu basi mti na matunda yake yatakuwa matunda mwitu tu, kutokana na mbegu uliyopanda. Wapo watu ambao maisha yao haya furaha lakini wapo watu ambao maisha yao yana furaha. Wanaokosa furaha siku zote huendelea kukosa furaha kwani mbegu waliyochagua huendelea kuwapeleka bondeni. Wanao furahia maisha huendelea kufurahia maisha maana mbegu waliyoipanda hundelea kuzaa na kutoa mbegu njema.

Tujifunze kutoka kwenye neno la Mungu: Mwanzo 1:11-12, Mungu akasema, nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake. Mungu akaona ya kuwa ni vyema.


Mpendwa msomaji, nchi hii ukilima mazao, ukipanda mahindi ni lazima magugu yatamea yenyewe bila kupandwa. Unakazana kwenye nini? kitu gani unapalilia? kama unapalilia magugu basi magugu yatakua lakini kama unapalilia mahindi basi mahindi yatakua. Watu wengi huwa wanapoteza furaha kutokana na hatua zake za maisha na kile ambacho unakizingatia.

Unaweza ukapanda mbegu mbovu lakini kama umestuka unaweza kupanda mbegu njema na ukaizingatia mbegu njema. Wakati Mungu aliumba hi dunia aliumba wanyama wakufugwa na wasiofugwa, miti ya kufugwa na isiofungwa. Ukifuga mnyama asiye fungwa, jiandae kwa maumivu. Ukifuga mti usiofugwa, basi jiandae kwa matunda ya mwituni.


Lakini wapo watu ambao maisha yao wanatamani sana kujiondoa kwenye hali ya kuwa mwituni kwao limekuwa jambo ambalo haliwekani licha ya kuwa hawataki kusumbuliwa na hali hiyo. Nalizungumzia hilo kwa sababu nimekubwa na hali hiyo kwa muda mrefu, licha ya kwamba nilipanda mti mwema lakini bado ile hali iliendelea kunifuata kwa sababu ipo na mimi, kama maneno matakatifu yanavyosema;  Yeremia 3:1, Watu husema, mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! mtu huyo atamrudia tena? Je! nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je!  utanirudia mimi? Asema Bwana.

Katika mazingira kama hayo wengi huteseka, wengi hujikuta wanafanya na wanaendelea kupalilia uovu hata kama hawataki. Mungu alipoiumba dunia aliikamirisha kila kitu lakini tatizo ni watu kuwana matumizi mabaya na vitu ambavyo Mungu amewaumbia na kuwapa wanadamu watawale. Mfano mdogo tu, ambao watu hutumia vibaya kile ambacho Mungu ameweka ndani yao, kama vile, dharau au kupuuzia. Dharau sio mbaya kwa mwenye matumizi mazuri lakini dharau ni mbaya sana pale ambapo unatumia kuwaumiza wengine. Lakini pia unaweza ukatumia dharau kuwasaidia wengine na kuepuka matatizo ambayo hayana maana. Luka 23:34, Yesu akasema, Baba, uwasamehe kwa maana hawalijui wanalolifanya. Huu ni mfano mzuri tu wa matumizi mazuri ambayo Mungu katuwekea vitu tutawale kwa bahati mbaya wengi humiliki.

Mpendwa msomaji; inawezekana mambo yako si mazuri katika maisha yako lakini kuna njia ya kutoaka. Haijarishi kuna kitu ambacho huwa kinakufinya na kukuumiza kiasi gani ndani mwako lakini yeyote yule ambaye yupo tayari kuchukua hatua Mungu ameweka uponyaji kwa kila mmoja. Watu wengi wanateseka kwa sababu wanataka wanavyotaka kwa sababu watu wanataka; lakini ngoja nikwambie hivi, chochote kile ambacho unakitaka utapata ikiwa tu utaanzia ndani yako na kukubali mazingra ya hapo ulipo kwamba nipo hapa sasa natubu kwa kufuata njia iliyo sahihi.

Kama umejikuta umeingia kwenye mtego basi kaa na utambue tu kwamba mtego sio mauaji bali ukinaswa kwenye mtego bado unamatumaini ya kuishi. Shukuru kwamba umepata makala ambayo itakusaidia na hali uliyonayo na kuanza kishi maisha ya matumini.

Mimi huhubiri injili ya maji na Roho lakini wakati nasoma kitabu cha ISHINDE TABIA YA KUGHAHIRISHA MAMBO, nilikutana na kanuni ya kupona kutoka kwenye hali hiyo na kanuni hiyo inaendana na ubatizo wa Yohana Mbatizaji, kanuni yenyewe ni;
Mfumo wa kutengeneza tabia yoyote mpya huwa unapitia hatua tatu, unatengeneza tabia yoyote ile ambayo unaitaka;
1.Kikumbushio.
2.Kitendo unachofanya.
Faida unayopata.
Huu ni utafiti wa kisayansi ambao unaweza kutumia kubadili tabia yoyote ile. Lakini nimekwambia kwamba utafiti huu unafanana kabisa na mahubiri ya Yohana Mbatizaji, formula ndiyo hiyo hiyo. Angalia, Mathayo 3:1-12, Siku zile Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea. Tubuni maana ufalme wa Mbinguni umekaribia. Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema. Sauti ya mtu inaita jagwani: Mtayarisheni Bwana njia yake, nyosheni barabara zake ,Yohana alivaa vazi lililoshonwa manyoya ya ngamia, na ukanda wangozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka pande zote za Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani. Lakini alopoona Mafarisayo wengi na masadukayo wanamjia, ili aawabatize aliwaambia, Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea mikimbie ghadhabu inayokuja? Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu.Msifikiri na kujisemea Baba yetu ni Abrahanu  hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya kuwa wototo wa Abrahamu. Basi,shoka lipo tayari kwenye mizizi ya miti; hivyo kila mti usiozaamatunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni. Mimi nawabatizeni kwa maji kuonyesha mmetubu. Lakini anayekuja baada yangu ananguvu kuliko mimi, nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Yeye anashika mkononi mwake chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano yake ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.


Yohana alikuja kuwageuza watu ambao walikuwa wamepotea, watu waliokuwa wanaabudu sanamu, watu wenye shida mbalimbali, watu wenye dhambi na hilo ndiyo kazi ya Yohana. Yohana alikuwa anawakumbusha kwamba uliko siko, tubu. Kutubu ni pale ambapo unakubali umekosea na unachukua hatua ya pili. Mpendwa msomaji, ili kuelewa hili kwa makini, kuna mambo matatu ambayo ni; imani, utayari na matumaini. Na siku zote hiyo ndiyo fomula ambayo kila mtu huwa anatumia kuishi. Rafiki yangu naomba uwe makini sana hapa; Labda nikufafanulie mstari wa kwanza na wa pili ili tuende kwa pamoja,...Siku zile Yohana Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea: Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia...[ hiki ni kikumbusho], kwa sababu watu walikuwa bize kufanya mambo yao ya hovyo, kufanya mambo yasiyofaa ambayo yapo nje ya uwepo wa Mungu sasa ilibidi Yohana awakumbushe hivyo. Sasa katika hiyo mbegu ndogo kabisa ya kikumbusho imebeba, mfumo wa imani, utayari na matumaini.

 Sasa kabla ya kuendelea mbele naomba nikuonyeshe mfumo wa Mbegu jinsi unavofanya kazi; MWANZO 1:11-12, Kisha Mungu akasema, nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu. Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Hizi ndizo hekima za Mungu, hakuna mtu anayetambua, mwanzo wa mambo yote ni yeye, asante, tuendelee.

Ukisoma mstari unaofuata utakuja kugundua kwamba, mbegu aliyokuwa anaihubiri Yohana, ilikuwa chanzo chake ni Mungu,  Mathayo 3:3, Huyu Yohane ndiye yule nabii Isaya alinena juu yake aliposema: Sauti ya mtu anaita jangwani: Mtayarisheni Bwana njia yake, nyosheni barabara zake. Kwa hiyo Mungu alitia neno ndani ya Yohana, mbegu aliyekuwa anaihubiri Yohana, mwanzo wake ni Mungu. Hareluya.

Sasa ukisoma kwa umakini kifungu kizima ambacho nimekuwekea hapo juu kinachohusu Yohana utakuja kugundua mfumo wake ndiyo huohuo. Sasa kwa kadili ambavyo anazidii kutoa ndivyo mambo yanazidi kuwa wazi wazi mpaka unakuwa msitu mnene.

Tutaendelea na makala na makala hii, kwa leo tuishie hapo. Lakini kitu kimoja ambacho rafiki yangu ningependa unisaidie kuwaalika watu ili tuwe pamoja katika makala hizi, alika kila mmoja kwa kumtumia makala hii. Hizi ni makala zenye uponyaji wa ndani kabisa kwahiyo hata wewe unapaswa kufuatilia mwendelezo huu ili uchimbe msingi kwa ndani zaidi. Makala hizi ni za uponyaji kiroho, kiakili na kimwili. Leo ndio tumeanza.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ▼  September (43)
      • Toa Ulichonacho, Anzia Hapo Ulipo.
      • Panda Mti Leo.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..13] Hatupokei Haki Ya Mungu...
      • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.
      • Usijikinai Ndugu, Utaoza.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..12] Injili Ya Maji Na ROHO....
      • Utukufu Ni Wa Mungu.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..11] Je! Ufanye Nini Wakati ...
      • Watu Hawatakosa La Kusema, Endelea Kufanya Unachop...
      • [TAFAKARI NENO YA LEO...10] Hamna Namna, Mshangaze...
      • Endelea Kufanya Yanayofaa.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO...9] Ukimpokea Yesu Onyesha...
      • Hii ndio Njaa Kubwa Ya Dunia Ya Sasa.
      • Tumia Makombo Ya Wakati Wako Kujisomea Neno La Mungu.
      • Naomba Uniambie Rafiki Yangu, Unaishije Na Watu Wa...
      • Una Shina La Kukupeleka Katika Ushindi.
      • Je! Mungu Atakuwepo Au Hatakuwepo?
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..8] Mambo Mawili Ambayo Huon...
      • Ukiona Unaliamini Jambo Na Huishi Hilo Jambo Basi ...
      • Je! Unapanda, Au Unashuka Bondeni?
      • Huwezi Kuuona Umuhimu Wa Maji Mpaka Visima Vikauke.
      • Kuijua Imani Na Kuishi Maisha Ya Ushindi.
      • Ukiona Fursa Hazigongi Mlango Jenga Mlango.
      • Jenga Tabia Hii Nayo Tabia Itakujenga Katika Mahus...
      • Gharama Ya KupataVitu Vizuri Vinavyokupeleka Katik...
      • [TAFAKALI NENO YA LEO...7] Ondoleo La Hofu Na Mais...
      • [TAFAKARI HEKIMA ZA WAZEE], Kuwaelewa Wengine, Kuj...
      • Alituchagua Tangu Tukiwa Na Dhambi. [Kwa Imani Tun...
      • Kanuni Ya Kibiblia Ambayo Inaweza Kukusaidia Kupan...
      • Utabiri Wa Nabii Danieli Juu Ya Injili Ya Maji Na ...
      • [TAFAKARI NENO YA LEO...6] Tumeandaliwa Mazingira ...
      • Umezaliwa Wa Kipekee Sana Lakini Watu Ndio Kioo Ch...
      • (TAFAKARI NENO YA LEO...5) Kama Una Tumaini Basi T...
      • Hakuna Mtu ambaye Hana Kabisa Katika Maisha.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO..4] Mtumainie Mungu Usikate ...
      • Hii Ni Bahati Yako Au Ni Wakati Sahihi Kwako?
      • [TAFAKARI NENO YA LEO 3] Usiende Kwa Mganga Siku Y...
      • Tunapokea Na Kutoa Kutokana Na Utayari Tulionao....2
      • [TAFAKARI NENO YA LEO...2] Je! Unataka Kuwa Na Fur...
      • Geuza Machungu Yako Kuwa Ushindi.
      • [TAFAKARI NENO YA LEO ...1] Jinsi Chuki Zinavyoene...
      • Tafakari Neno Ya Siku.
      • Tunapokea Na Kutoa Kwa Utayari Tulionao.
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates