JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Wednesday, January 1, 2020

Uhuru Wa Kufanya Mambo Na Mipaka Yake.

 Sadick Kilasi     January 01, 2020     No comments   

Uhuru Wa Kufanya Mambo Na Mipaka Yake.

Katika maisha kila mmoja anahitaji uhuru. Haijarishi ni mtu wa namna gani awe mkubwa ama mdogo, uhuru ni jambo la muhimu kwa kila kiumbe chochote kile.

Ushawahi kumipinga sisimizi  mbele yake, katika mwenendo wake? Hakika ukiwapinga siafu katika msafara wao hukasirika sana.

Maisha ni uhuru, na hapo ndipo maisha kwako yanaweza kueleweka. Haijarishi upo katika wakati upi lakini kama unaona njia mbele yako hata kama unawakati mgumu bado utakuwa na matumaini na furaha.

Kila kiumbe katika maisha kinatafuta Uhuru.  Hatupendi kuzongwazongwa sisi viumbe ambao tumeumbwa na Mwenyezi Mungu. Kama sisimizi hapendi kuzongwazongwa, yeye aliye kiumbe mdogo sana, je! sisi tulio viumbe wakubwa wenye akili zaidi? Kila kiumbe hupenda kiendeshe maisha yao kama chenyewe kinavyota.

Nenda kamchunguze jongoo, umtinge mbele yake, uone atakavyokasirika. Hakika atakasirika.

Ijapokuwa kila kiumbe anapenda uhuru, lakini uhuru usio na mipaka, huleta uharibifu.  Jongoo ni mmoja wa viumbe ambavyo havioni vizuri lakini hapendi kuingiliwa na kutingwa mbele. Anapohisi utofauti wa kutingwa hukasirika sana.
Lakini jongoo huenenda bila mipaka, kitu ambacho kinamfanya utamkuta ndani ya nyumba ya mtu, sasa huu ni uhuru uliokosa mipaka.  Tunahitaji kukosolewa ili tuone kosa letu.


Uhuru mkubwa ni wa muhimu, na kukosolewa kidogo inafaa. Sisi wenyewe ndio tunaotafuta uhuru, na mazingira yetu hupinga uhuru. Si kwamba yanakuwa yanapinga uhuru wetu bali sisi wenyewe tunakuwa tumeingilia uhuru wa mazingira. Kila kiumbe kimepewa mazingira ya kutawala, na mipaka yake.

Naam, kitu cha muhimu cha kutambua katika maisha ni Uhuru wa wakati wote.  Huu ni uhuru ambao haungiliki na chochote.  Hata mazingira hayawezi kuadhiri uhuru huu. Uhuru wa kimtazamo ambao unaendeshwa na maamuzi, ni uhuru wa ndani yako. Katika mazingira yoyote unaweza kufanya maamuzi huru wakati unatingwa ama kuzuiwa mbele.

Tulizaliwa tukiwa tumeyakuta mazingira yakiwa yapo, tukataka kutaka kuona ni namna gani ambavyo tunaweza kwenda sawa na mazingira na kutumia vile ambavyo tunahitaji.

Lugha ambayo tunazungumza hatukuzaliwa nayo, bali tumeikuta ikiwa ipo, tukajifunza na tukaenda nayo sawa.

Kwa hiyo, chochote ambacho unakutana nacho mbele yako ni kama kuzaliwa katika nchi usiyoijua, kwahiyo unapaswa kwenda sawa na yale mazingira ama nchi.

Maamuzi utakayofanya yatakuwa maamuzi huru kutokana na mazingira uliyopo, na kiwango cha uhuru huohuo.

Basi, uhuru ni wa muhimu katika maisha. Kila kiumbe kinahitaji uhuru. Angalia jinsi gani ambavyo unaendesha uhuru wako. Nguvu ya uhuru ipo katika mitazamo yako.

Kuna siri moja ambayo nataka nikupe, Leo, hapa.  Kuna uhuru wa akili na kuna uhuru wa hisia. Uhuru wa akili ni uhuru wa wewe kwenda sawa na mazingira. Uhuru wa hisia ni uhuru wa wewe kuendeshwa na mazingira.  Uhuru huu wote ni sawa, kwa wakati.

Asante.


jikolaushauri.blogspot. com.

Sadick Lazaro Kilasi.
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ▼  2020 (5)
    • ▼  January (5)
      • Falsafa Za Asili: Jiwe Lililirushwa.
      • Meli Kuelea Juu Ya Maji.
      • Pembe Tatu
      • PENDO LA HEKIMA.
      • Uhuru Wa Kufanya Mambo Na Mipaka Yake.
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ►  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ►  October (29)
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates