Zaburi 34:11-22, Njoni, enyi wana, msikilize, nami nitawafundisha kumcha Bwana. Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima, apandaye siku nyingi apate kuona mema? Uuzuie ulimi wako na mabaya, na modomo yako na kusema hila. Uache mabaya na ukatende mema, utafute amani ukaifuatie. Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, nna masikio yake hukielekea kilio chao. Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya, aliondoe kumbukumbu lao duniani. Walilia, naye Bwana akasikia, akawaponya na tabu zao zote. Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, na walio pondeka roho huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana humponya nayo yote. Huihifadhi mifupa yake yote, haukuvunjika hata mmoja. Uovu utamwua asiye haki, nao wamchukiao mwenye haki watahukumiwa. Bwana huzikomboa nafsi za watumishi wake, wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.
Mwenyezi Mungu wale wlio kata tamaa, wale walio vunjika mioyo yao, wale wasi na tumaini, wale walio pondwa roho zao. Mungu anaseama, Njoni enyi wana, msikilize nami nitawafundisha kumcha Bwana. Kama unataka uzima, kama unataka kufurahia maisha siku nyingi, Mungu anakuita, anataka akufundishe njia zake, anataka akuonyeshe hekima zake, maana kumcha Mungu ni mwanzo wa hekima na busara.
Chukua hatua rafiki yangu, anza maisha mapya, mtafute Mungu tena kwa bidii, maana yeye hukomboa nafsi zinazomtafuta yeye. Katika tafakari neno hii ya leo hakikisha unaenda hatua ya ziada. Uvae utayari leo unafaa, fanya maamuzi badili maisha, anza kuwa na tumaini na usiishi kama mfu, usibebe jeneza la maiti kwa sababu kwa sababu ya kukosa tumaini, maana mtu ambaye hana tumaini amekufa, kwa sababu watu tunaishi matuini yetu na ndio maana tupo. Yeyote anayetumainia kufa amekufa na yeyote ambaye anatumainia uhai yupo hai. Mungu ndiye tumaini letu sisi tulio hai kwa sababu yeye ni hai na hafi.
Rafiki chukua hatua, Mungu alimtuma mwanaye Kristo Yesu ili kila anayemwamini yu na uzima wa milele. Na ndiomaana nimeandika kitabu cha UKRISTO NA MAISHA, kwa ajili yako wewe rafiki yangu. Kitabu ambacho nimeelezea juu ya funguo za Ufalme wa Mungu kupitia injili ya Maji na Roho ambayo ndio ufunguo wa ufalme wa Mungu. Hakikisha unajipatia kitabu hiki bure kabisa, wewe nitumie ujumbe wa meseji [email] au whatsapp, nitakutumia kitabu. Pia karibu katika group la whatsap ili tuwe tunashirikishana tafakari za kila siku.
Nisaidie kusambaza makala hii kwa marafiki zako pia, hili ni ombi langu kwako, asante.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment