Mathayo 4:3-4, Mjaribu akamjia akamwambia, ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akamjibu akasema, imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu, nimeona kwamba sasa nitakuwa nakushirikisha kila siku mambo ambayo nitakuwa nimejifunza kwa siku husika. Nitakuwa ninaandika makala ambayo nitakushirikisha mambo ambayo nimejifunza kutoka kwenye kusoma Biblia, ama katika mapito ambayo nimepitia katika siku husika.
Kwa sababu nipo hai lazima ninamapito ya siku, ningalikuwa nimekufa basi ningalikuwa sina tafakari ya siku. Kwa hiyo ile kanuni yetu ya NDANI, NJE nitakuwa nakushirikisha makala ambazo nimejifunza kwa siku husika. Furaha yangu ni kwamba, binafsi nitakuwa na zoezi la kujenga nidhamu na uadilifu, nitakuwa naweka kumbukumbu za maisha ambazo zitaendelea kunisaidia baadae lakini pia litakuwa ni jambo zuri sana mimi na wewe kujifunza kwa pamoja yale mambo ambayo tunapitia kwa siku.
SOMA:KUTUMIA SHERIA YA NDANI, NJE, KUTATUA TATIZO.
Kwa hiyo rafiki karibu katika tafakari zangu ili tuweze kujifunza kwa pamoja kwani hata wewe unalo la kujifunza na kunishirikisha mimi. Kwa mpango huo sasa, karibu katika Group letu la SURA YA UKWELI ili tupate kushirikiana na kujengana kutokana na mapito yetu. Kitu cha muhimu ni hiki, wewe kutafakari yale ambayo umejifunza na kupitia kwa siku kwa ni hilo ndilo neno kutoka kwa Mungu.
Karibu sana kwenye GROUP LA SURA YA UKWELI, tujofunze kwa pamoja. Kumbuka, Mimi ni zawadi yako na wewe ni zawadi yangu mimi.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni sadikila65@gmail.com au 0687000768.
0 comments:
Post a Comment