Je! utafanya nini wakati ambao mambo hayaendi kama vile yanavyopaswa kwenda? Utafanya nini pale ambapo unapaswa kuvuka kiunzi kilichowekwa mbele yako ili kikupime ulivyo na ubunifu?
Kutoka 15:23-26, Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa maji yale ya Mara; kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hiyo jina lake likaitwa Mara. Ndipo watu wakamnung'unikia Musa, wakisema, tunywe nini?Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko; akawambia, kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kushika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nikuponyaye.
Kitu ambacho unapaswa kuelewa wakati unapitia magumu ni kwamba , wakati huo ni wakati wa kujengwa, wakati wa kujifunza. Lakini lazima uelewe kwamba, Mungu ameweka kanuni ambayo unapaswa kuifuata ili kusikia sauti hii wakati huu mgumu.
Kwanza kabisa Mungu amesema, unahitajika kuwa mtulivu sana, na utasikiliza kwa bidii sana sauti ya Roho Mtakatifu, na kufanya lile jambo ambalo Mungu amekuelekeza ufanye. Sasa hapa lazima utambue kwamba, unahitaji utulivu mkubwa sana na ile sauti ya kwanza ambayo Mungu kakuonyesha uifanye ndiyo hiyo hiyo. Unatulia kimya harafu kitakacho kuja ambacho umesikia kutoka ndani kabisa ya Roho yako hicho ndicho ufanye.
Lakini lazima utambue kitu kimoja, kwamba lazima uwe mtu ambaye unazitii sheria za Mungu na maagizo yake. Ni lazima kwanza uwe unamwamini Mungu na ndipo utapata kile ambacho unahitaji.
Kwa hiyo magumu katika maisha yapo lakini kwa watu ambao wanautayari wa kuishi na kukubali mazingira wanayopiti hawahesabu, wakati huu kama wakati wa kujijenga. Tunajijenga kupitia magumu, sasa kama unafikiri kufurahi wakati wa mema pekee, basi, hapa unahitaji kuelewa hili kwamba, wakati wote ni sahihi kwa mwenye shukrani na kuona wema kwenye kila jambo.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment