Kutoka 16:17-18, Wana wa Israeli wakafanya hivyo, wakaokota wengine zaidi, wengine kupungua. Nao walipopima kwa pishi, yeye aliyekuwa ameokota kingi hakubakiwa na kitu, na yeye aliyekuwa ameokota kichache hakupumgukiwa; wakaokota kama ulaji wake ulivyokuwa.
Inawezekana una uchungu ndani mwako wa wivu ambao umekuwa mzigo kwako na tamaa fulani zinakusumbua katika maisha yako lakini rafiki, ndugu, wewe nikuhakikishie tu kwamba ukiona huna inamaana unacho. Chochote ambacho huwa unafikiri huna basi hicho ndicho ulichonacho. Na chochote kile ambacho unafikiri unacho basi hicho ndicho huna.
Luka 17:33, Mtu yeyote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na yeyote atakaye iangamiza ataiponya.
Katika maisha tumewekwa tutegemeane katika maeneo mbalimbali na hii inategemea utofauti wetu tulionao. Fikiri kitu kimoja rafiki yangu huwezi hata kujiangalia vizuri uso wako lakini mwenzako anaweza kukuangalia kwa ubora zaidi kuliko wewe mwenyewe binafsi. Kama wewe ni moja kati ya watu ambao huwa unawalinganishia watu vitu fulani ambavyo unavimiliki basi kaa na utambue kwamba unawalingishia wenyenacho.
Maskini na umaskini wako usijidai na umaskini wako kwani umaskini huo sio wa kwako. Tajiri na utajiri wako usijidai na utajiri wako kwani utajiri huo sio wa kwako.
Waebrania 13:10, Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake.
Mpendwa rafiki, Mungu anakupenda sana wewe na ndiomaana amekupa hao majirani zako. Fikiria namna ambavyo umepewa mwili ili wao wakutazame, fikiria namna ambavyo wao wamepewa mwili ili na wewe uwatazame wao. Mheshimu alipo jirani yako kwani yeye ni kioo chako. Wakati mwingine unapaswa kumpa pongezi na kumwambia hivi, wewe ni zawadi yangu, na yeye ni zawadi yako.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment