Yakobo 2:14,26, Ndugu zangu yafaa nini, mtu akisema ya kwambaanayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo natendo imekufa.
Chochote kile ambacho unakiamini basi unapaswa kuishi wakati huu wa sasa. Tunaishi dunia yenye mambo mengi sana, matukio hutukia kila baada ya sekunde, kifo nacho kipo jilani sana kuliko uhai kwahiyo chochote unachokiamini ishi hicho unacho kiamini.
Usisubiri ukamirifu, ukamirifu haupo hapa duniani kwahiyo kazana kuishi kile ambacho unakiamini. Usingoje mpaka uwe na kitu fulani ama kianzio fulani, hapana, fanya kitu ambacho unakiamini huku ukizingatia msingi wa hapo ulipo. Kunali mazingira uliyopo kisha songa mbele.
Ukipiga hatua kutoka hapo ulipo, utasimlia watu kutoka hapo ulipo. Usijidanganye mwenyewe, chukua hatua. Kama unataka kusoma kitabu basi chukua hatua soma, kama unataka kumsamehe mtu basi chukua hatua samehe, chochote kile ambacho unataka kufanya fanya.
Hakuna imani bila matendo, kama unaliamini jambo harafu hulitendi wewe unalitambua tu, huliamini. Ishi unachokiamini.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment