Siyo kwa binadamu kujitaidi kwa matendo yake, hapana, ila, alitaka kila mmoja anayemwamini Yesu apate kuokolewa. Haitegemei kwamba, utoe sadaka nyingi sana kanisani, hapana, haitegemei kuwa mtenda mema, hapana, ila kwa imani. Unapoamini kwamba Mungu alitoa mwanae Yesu Kristo ili achukue dhambi zako, hapo ndipo unapata haki ya kutimiza mapenzi yake. Unapoamini kwamba Yesu ni Kristo, kwa imani utatekeleza mapenzi ya Mungu na siyo wewe ambaye utakuwa unatekeleza mapenzi yake.
Imani huwa ndani ya mtu, Rohoni, kwenye moyo wa mtu na huko ndiko mtu huanza kutekeleza matakwa na nje matendo hutokea. Mungu huwahukumu watu ndani ya mioyo yao na sio matendo ya nje. Moyo wa mtu huamini na ukisha kuamini hupokea haki na kukiri waziwazi.
Watu wote ulimwenguni wamesamehewa dhambi zao, si Mkristo, si Mpagani, si Budha, si Muslamu na si dini nyinginezo. Dhambi za watu wote ulimwenguni zilichukuliwa na Yesu katika mto Yordani pale alipobatizwa na Yohana, Yohana kama kuhani wa wanadamu na Yesu kama mwana kondoo aichukuae dhambi ya ulimwengu na kwaajiri ya dhambi hizo aliteswa msalabani, akafa, akafufuka kwa uweza wa Roho wa Mungu na sasa yupo hai anawabatiza watu kwa Roho Mtakatifu.
Hivi leo tunaliamini tendo lilofanyika katika mto Yordani miaka 2000 iliyopita dhambi zote za ulimwengu zilichukuliwa na yeyote anayeamini hivo atapokea haki kutoka kwa Mungu na kutiwa chapa ya Roho Mtakatifu. Yesu yupo hai, kuwabatiza watu wote ambao huamini kwamba, dhambi zao zilichukuliwa na yeye.
Unapoamini hatua hizi, ni rahisi kutekeleza amri za Mungu kwani tayari umefanyika mwana wa Mungu. Yohana aliwambia watu hivi, tubuni, na kuonyesha kwamba mmetubu onyesheni kwa matendo, mwenye nguo mbili ampe asiye na nguo, usitoze zaidi ya inavotakiwa. Sio tendo la kufanya tu kuonyesha matendo mema, hapana chanzo chake ni Mungu. Mungu ndiye mwanzo wa mambo mema.
Mungu hawahukumu watu kwa matendo yao ya nje bali kwa kile ambacho umedhamilia ndani ya moyo wako. Kwa hiyo kama wewe ni mnafki kwa nje Mungu atahukumu kutokana na moyo wako ulivo dhamilia. Pale ambapo umefanyika mwana wa Mungu ni rahisi kutekeleza matakwa ya Mungu kwa sababu wewe ni mwana wa Mungu na umeushinda ulimwengu.
Ukombozi ni kwaajili ya wote, na alama ya ukombozi ni kupokea Roho Mtakatifu, na ufunguo wa kupokea Roho Mtakatifu ni kuamini katika, maji, damu na Roho. Maji, ubatizo wa Yesu aliobatizwa na Yohana,damu, mateso ya Yesu msalabani, ikimaanisha, upatanisho na Roho ni kifo na ufufuko wake.
Yeyote anayeamini na kukiri kwa kinywa chake atapokea wokovu na kuonyesha kwamba umeamini na umekiri, tekeleza mapenzi yake, ambayo ni, imani kwake na upendo kwa watoto wake. Mpende Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote na upende jilani yako kama unavojipenda mwenyewe. Epuka maisha ya lawama bali siku zote, mtangulize Mungu kwa kila jambo na uishi kwa shukrani siku zote. Asante.
Rafiki yangu nisaidie kusambaza hizi makala, share kwa marafiki zako ili watu wapate kuponywa mioyo yao. Nakuomba rafiki yangu. Asante kwa kusoma makala hii Mungu akubariki.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment