Dunia ipo chini ya utawala wa nguvu hasi, nguvu hiyo ndiyo nguvu ambayo ndani yake kuna hofu, kiburi, ubinafsi na hali mbalimbali za mfadhaiko. Wakati dunia inaumbwa giza tayari lilikuwa linatawala, sasa nuru ilipoletwa giza iliifia nuru. Si kwamba giza liliondoka moja kwa moja, hapana, nuru ilipata nguvu kwenye giza.
Mwanzo 1:2-4, Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tene utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa virindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru ya kuwa ni njema; Mungu akaitenga nuru na giza.
Giza lilikuwepo lakini Mungu alipambanua alipoirusu nuru, akabainisha kwamba, nuru ni njema. Baada ya hapo Mungu aliendelea na kazi yake huku, huku nuru ikawa ndiyo inayomwongoza. Nuru ilikuwepo kwa sababu giza lilikuwepo na sasa nuru ipo kwa sababu giza lipo.
Mpinzani mkubwa sana wa maisha ya furaha ni hofu. Na hofu asili yake ni giza na furaha asili yake ni nuru. Kuna mambo mawili ambayo ndiyo msingi wa maisha ya mtu ambayo hutupilia mbali hofu na mafadhaiko.
1.Kujifunza Neno la Mungu na tafakari mbalimbali.
Moja ya kitu ambacho nimejifunza kutoka kwa maisha ya Yesu ni hiki; Mafarisayo na Walimu wa sheria, walikuwa wapinzani wakubwa sana wa Yesu.Toka Yesu anaanza kazi yake walikuwa wanajaribu kumtega na kumkamata lakini ilikuwa inashindikana. Mafarisayo katika neno la Mungu, walitumika kama wapinzani, inamaana walikuwa ni watu wa giza. Walimjaribu Yesu ili awe adui yao lakini ilishindikana, Yesu alikuwa anawachukulia kwa jinsi walivyo na alikuwa anawatumia kuwafunza wengine. Ikiwa utafuata nuru na kuondoa mtazamo wa uadui si rahisi hofu kukuingi. Lakini pia, Yesu alipokuwa anawafundisha watu walikuwa wanashindwa kumnasa kwa sababu neno lake lilikuwa ni nuru na mitego yao ilikuwa inashindwa. Ikiwa utachukua neno la Mungu na kujifunza unakuwa unaingiza nuru ndani yako na giza lenyewe litahama. WAEFESO 5:26, Ili makusudi alitakase na kusafisha kwa maji katika neno. Kwa kadili ambavyo unasoma neno la Mungu ndivyo dhamiri yako inatakasika. Na giza linaondoka ndani mwako.
2.Upendo.
Moja ya jambo kubwa kabisa ambalo hofu haiwezi kuingia kabisa basi ni upendo. Penye upendo wa kweli hata magonjwa hayawezi kuingia. Siku ambayo Yesu alitiwa mbavuni na maadui zake ni siku ambayo watu wote walimtenga. Wakati watu walipokuwa wanaunganika kwa pamoja kwa upendo Yesu hakukamatwa. Yesu aliwatibu watu magonjwa, watu waliokuwa wametengwa kama wenye ukoma lakini kwa sababu ya upendo alishinda hayo yote. Penye pendo hapana hofu.
Sababu hizi mbili ni msingi ya Neno la Mungu yaani amri kuu mbili; Mpende Bwaba Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa nguvu yako yote. Mpende jilani yako kama unavojipenda wewe mwenyewe. Kwa hiyo ni vema tukajitahidi kukua katika kusoma neno la Mungu na kuishi kwa upendo na watu. Asante.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment