Kama unachofanya hakikuumizi mwenyewe wala hakimuumizi mwingine, fanya, hata kama utapokea maoni ambayo yapo kinyume na wewe na kwa asilimia themanini maoni yatakupinga.
Ndugu yangu, kuna mtu alipingwa kama Yesu? Alipigwa bila makosa yoyote. Dunia inataka kufanya kile ambacho kimezoeleka na wao lakini ukija na jambo jipya watu watakupinga na kukuona hufai kabisa.
Mathayo 11:16-19, Basi, nitakifananisha kizazi hiki na kitu gani?Ni kama vijana waliokuwa wamekaa uwanjani, wakawa wakiambiana kikundi kimoja na kingine: Tumewapigieni ngoma lakini hamkucheza! Tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkuomboleza! Kwa maana Yohane alikuja, akafunga na wala hakunywa divai, nao wakasema: amepagawa na pepo. Mwana wa mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema, rafikiao watoza ushuru na wenye dhambi!Hata hivyo, hekima ya Mungu itadhibitisha kuwa njema, kutokana na matendo yake.
Kama hao walipingwa na ndio hao leo hii wamefanya sisi kutokuwa na dhambi, je! wewe kwanini usipingwe? Endelea kufanya kwa sababu unapaswa kufanya, endelea kufanya kwa sababu unajenga watu, endelea kufanya kwa sababu malengo yako ni kujenga na wala sio kupomoa. Siku moja unachokifanya kitathibitisha kwamba kusudi lako lilikuwa ni nini?
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment