Kama unawasiwasi kwamba Mungu yupo au hayupo, nitende mema au nisitende mema, kwa ushauri wewe tenda mema. Hata kama huna uhakika wa kumkuta Mungu wewe tenda la kufaa. Ukitenda la kukujenga ni faida kwako na ukitenda la kukubomoa ni hasara kwako, si bora utende lililo jema, usimkute Mungu lakini usiwe na cha kupoteza. Lakini kama ukitenda uvu, harafu ukamkuta Mungu basi ni wazi utakuwa umepoteza hapa duniani na peponi pia.
Mungu kaweka kanuni ambazo zinawafanya wale ambao wanamtumainia wawe na uhakika na uwepo wake. Asili ya mbegu mwitu na matunda yake huwa mwitu na asili ya mbegu njema na matunda yake huwa matunda mema. Hii ni kanuni ya Mungu ambayo kaiweka hapa duniani na watu ndzo kanuni tunazoziishi.
Mungu asili yake ni nuru, yaani mwanga. Nyota tumaini lake kuwa kama mwezi, na mwezi tumaini lake kuwa kama jua na jua tumaini lake kwa Mungu. Hii ni kanuni ya nuru ambayo Mungu kaweka duniani.
Wajinga wenye matumaini tumaini lao kuwa wenye haima na wenye hekima tumaini lao ni Mungu. Mungu ndiye mwisho wa kila jambo. Ndiye tumaini la mbingu na nchi, maana yeye ndiye aliyefanya upacha huu.
Mungu alifanya nuru na giza.
Mungu alifanya usiku na mchana.
Mungu alifanya maji ya chini na juu.
Mungu alifanya mbingu na nchi.
Mungu alifanya mvua na ukame.
Mungu alifanya mwamme na mwanamke.
Mungu alifanya wanyama mwituni na wanyama wa kufugwa.
Mungu alifanya samaki na wanyama.
Mungu alifanya bahari na nchi kavu.
Mungu alifanya leo na kesho.
Mungu alifanya jua na mwezi.
Mungu alifanya nyota na giza.
Mungu alifanya hofu na furaha.
Mungu alifanya Adamu na Yesu.
Mungu amefanya watu na yeye.
Mungu yupo rafiki yangu, kazana kutenda linalofaa kutendwa na wewe utapokea tuzo lake. Mfanye yeye kuwa imani yako, ngao yako na tuzo lako. Mungu anatupenda sana.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment