KANUNI YA IMANI.
Cha kwanza kabisa kila kitu ambacho kipo duniani huendeshwa kwa imani tu. Vitu vyote vyenye sura ya kueleweka huwa havieleweki. Sasa kwa sababu havieleweki basi lazima lugha yenye mipaka lazima itumike. Vitu vyote vyenye mwili huendeshwa kwa imani tu na sio ukweli halisi. Majina yao ni majina ya kukalili au majina ya kuzoea, wasomi wanaita mantiki. Na ndiomaana ni rahisi mtu kubadili jina lake lakini uhalisia wa sura yake haupotei, naweza kubadili jina langu la Sadick labda kwenda jina la Antoni na baadae jina hilo likazoeleka na watu wakawa wanalitumia vizuri kama jina la mwanzo lakini mwanzo nilikuwa naitwa Sadick na watu walikuwa wamelizoea jina hilo. Ili ukweli wa majina uwe ukweli lazima nitumie imani. Imani huwa inabadilika lakini ukweli huwa haubadiliki. Kwa kadili ambavyo unajua kitu ndivyo ambavyo utazidi kubadili imani yako. Imani yako inawezekana ikawa inaongezeka au inapungua kutokana na ukamili wa taarifa na jinsi ambavyo unachukulia hilo jambo. Ni muhimu sana kuelewa juu ya imani kwani vitu vyote nyenye mwili huendeshwa kwa imani tu kwani kila kitu chenye mwili hakieleweki kilikotoka. Dunia hujaza sehemu ambayo inautupu na ikisha kujaza mwanadamu atakipa jina kile kitu; mfano, mti, nyasi, watu na kila kitu chenye mwili. Imani ni maoni ya mtu juu ya jambo fulani.
Imani ni kuwa na hakika na mambo yajayo, hii ni maana ya kibiblia. Waebrania 11:1, Kuwa na imani ni kuwa na hakika na mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona. Ikiwa tupo duniani na tunaona kila kitu, je, tutakuwaje na imani? Na kwa sababu imani ni kuwa na hakika na mambo usiyoyajua basi ni wazi kwamba kila kilichopo duniani hakina ukweli ulio sahihi. Na tunaamini kwamba hii ndio dunia ya kueleweka, mambo yote hapa yapo waziwazi tofauti na rohoni ambako kwa imani inasemekana kwamba huko hakuna vitu vyenye mwili.
Waebrania 11:3, Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana. Kwa sasa tupo katika dunia ya vitu vinavyoonekana na tumaini letu ni kuona uso wa Mungu ambapo ndipo mwanzo wa dunia kuumbwa kwani dunia iliubwa kwa neno la Mungu. Kwa sasa tupo kwenye vitu vinavyoonekana tunarudi sasa kwenye vitu visivyoonekana. Lakini kwa kuwa bado tupo safarini katika dunia hii tunaweza kuwa na hakika kutoka vitu visivyoonekana kwenda kwenye vitu vinavyoonekana, hiyo nayo ni imani. Waebrania 11:11, Kwa imani hata Sara aliamini kwamba Mungu hutimiza ahadi zake, kwa hiyo akajaliwa kuchukua mimba ingawaje alikuwa amepita umri. Imani ni kupata haki ya jambo ambalo halipo. Na hivyo ndivyo dunia inakwenda kwa imani. Watu wote tunaishi kwa imani, kutoka kwenye kitu kisichoonekana kwenda kwenywe kitu kinachoonekana na kutoka kitu kinachoonekana kwenda kwenye kitu kisichoonekana. Haya yote ni matumaini ambayo tunayo. Imani ni kufanya jambo kuwa haki amblo halina hakika kuwa kweli. Kila jambo limefichwa, ukiona unacho basi tambua wakati wote kile kitu ambacho unacho kinaweza kuchukuliwa na ukiona huna basi tambua kwamba ukiwa na imani tu na kupata haki ya kile ambacho huna utapokea kutoka kwa Mungu. Katika dunia tunaishi ndani ya wakati, vitu vyote vyenye mwili kwa kadili wkati unavokwenda hupoteza ubora wake na mwisho hupotea kabisa lakini hivyohivyo tena sehemu ambayo ipo wazi ni lazima ijazwe kutoka kwenye vitu visivyoonekana kwenda kwenda kwenye vitu vinavyoonekana na hii ndio imani. Lazima utambue kwamba vitu vya mwili na vya rohoni haviwezi kukaa kwa pamoja, ni jambo ambalo haliwezekani ni lazima mwili utumainie rohoni na rohoni kutumainie mwilini. Sasa kutokana na kutokuwepo kwa ukamirifu huo basi imani lazima itumike, na hapo ndipo ambapo mtu anajenga picha kichwani mwake ya jambo ambalo halipo katika uwepo wa macho.
UMUHIMU WA IMANI KATIKA MAISHA.
Ikiwa umetambua tayari kwamba maisha ya hapa duniani hayana ukamirifu basi ni wazi kabisa tayari umeuona umuhimu wa imani. Kama chenye mwili huingia duniani na kuanza kupoteza kila wakati, kutoka kwenywe kwenye kuwepo kwenda kwenye kutokuwepo basi ni wazi kwamba ni muhimu sana kujali wakati au muda. Ni muhimu sana kujali wakati, kwa sababu kila sekunde kwako ni gharama ya maisha yako inapungua. Ikiwa kila sekunde unamegwa na kuondolewa sehemu fulani ya uzima wako basi mwisho uzima utakuishia na wewe utabaki huna cha kuishi katika ulimwengu, mwili wote umeisha. Sasa kama wakati sio kipaumbele chako basi tambua kwamba utaenda kama ulivokuja bila kuacha alama yoyote hapa duniani.
Kitu kingine cha muhimu katika imani ni kutambua mazingira na kujitambua mwenyewe. Unajua, unavojielewa kwamba wewe ni mwili na unamatumaini ya kurudi rohoni ni wazi kwamba tayari utaishi kwa matumaini ya kwenda rohoni. Hivi sasa watu wengi wanaishi maisha ya kutumainia kwenda rohoni. Kwa kuwa unatambua abisa kwamba utakwenda rohoni basi bi wazi kwamba lazima ubaki kwenye njia ya kwenda rohoni, njia ambayo itakurudisha ulikotoka na sio kwenda jehanamu ambako hujatoka huko, hana, ni lazima ubaki katika njia kuu.
Kitu kingine cha muhimu kwenye imani, ikiwa tayari umeelewa imani ni nini? Tayari unaweza kutambua kwamba, hapa, hapa, duniani kama ulikuwa umekosa kitu fulani ni wazi kwamba unaweza kumwomba Mungu na akakupatia kile kitu ambacho huna na ukakipata kwa sababu chochote kile ambacho huna ukimwomba Mungu anakupa. Mwanzo 15:1-6, Baada ya mambo hayo neno la Mwenyezi Mungu lilimjia Abramu katika maono, Abramu! usiogope! Mimi ni ngao yako. Tuzo alko litakuwa kubwa! Lakini Abramu akasema, Ee Mwenyezi Mungu, utanipa nini hali naendelea kuishi bila mtoto, na urithi wangu ni Eliezeri wa Damasko? Tazama! Hujanijalia mtoto; mtumwa aliyezaliwa nyumabani mwangu ndiye atakaye kuwa mrithi wangu! Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia, Huyu hatakua mrithi wako! Mwanao halisi nndiye atakayekuwa mrithi wako. Hapo Mwenyezi Mungu akamleta Abramu nje na kumwambia, Tazama mbinguni, zihesabu nyota, kama kweli utaweza kuzihesabu! Hivyo ndivyo wazawa wako watakavokuwa wengi! Abramu akamwamini Mwenyezi Mungu, naye mwenyezi Mungu akamkubali Abramu kuwa mwadilifu.
Mungu alimkubali Abramu kwa imani na alimkubali Abramu kuwa mwadilifu kwa imani tu kabla ya matukio kutukia na Abramu alimwamini Mungu kwa imani tu kwani Abramu alikuwa bado hana uzao wa kumrithi na wala Mungu alikuwa hajamtimizia ahadi. Unapo amini, unapokea haki na ukisha kupokea ndipo matokeo nje huonekana. Leo hii hata sisi Abramu ni Baba yetu wa imani kwani yeye ndiye mwanzo waimani. Waisraeli pekee ndiyo waliokuwa taifa teule la Mungu lakini hata sisi tunashiriki kuwa watoto wa Mungu kwa imani. Maisha ya Abramu yalikuwa hayana tumaini lakini kwa imani akapata tumaini jipya ambalo Mungu alimuahidi.
Lakini faida nyingine ndiyo hii, ni njia nzuri zaidi ya kuondoa uchungu moyoni mwako ikiwa unamatatizo fulani. Ni rahisi kumsamehe mtu moyoni mwako kuliko kumkabili nje. Ikiwa utaanza kuwasamehe watu na kujisamehe mwenyewe basi tayari unakuwa unaukomavu wa ndani. Ni rahisi kuomba maombi mengi rohoni mwako, laakini pia ni rahisi kutimiza jambo ambolo linaanzia ndani na kutoka nje. Ikiwa unataka kutimiza mapenzi yako kwa matokeo ya nje basi ni wazi kwamba ndani mwako uwe unahamu zaidi ya mara mbili ya matokeo ya nje, ili utimize vizuri. Mathayo 5:20, Ndiomaana nawambieni, wema usipozidi ule wa walimu wa sheria na wa mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Ikiwa unataka kufanya jambo lolote basi inatakiwa uwe na hamu kubwa ndani yako harafu nje utatimiza kwa ubora zaidi kwa kadili ya imani yako. Mafarisayo na walimu wa sheria ni walikuwa watu ambao hutimiza mambo yao kwa kinafki kwa sababu walikuwa hawana imani ndani yao, sasa Yesu alimbia watu msipozidi kuwa na hamu kubwa zaidi ya walimu wa sheria na mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Ni lazima uwe na hamu kubwa ndani mwako ya kutaka kuwa bora, ni lazima ndani mwako uwe na hamu kubwa ya kutaka kuishi na watu vizuri na watu, ni lazima ndani mwako uwe na utayari wa kutaka kujijenga zaidi hata kama watu nje wanakuonyesha na kukukatisha tamaa.
Hii ni sheria, kwamba lazima uwe na imani ndani mwako na ndipo utimize mapenzi yako. Ikiwa unajengeka ndani mwako kwa imani kwa mtu ambaye hawezi kuona basi ni rahisi kujengeka kwa nje ambako watu huona. Kama ukiwa tayari kujielewa wewe mwenyewe basi ni rahisi kuwaelewa wengine. Kama ukiwa tayari kujihimili wewe mwenyewe basi ni rahisi kuwahili wengine. Ukitimiza haya basi huo ni utajiri. Lao Tsu. Ni ukweli mtu, ukiweza kujijenga wewe mwenyewe binafsi basi rahisi kuwajenga wengine na ukiweza kujielewa wewe mwenyewe binafsi basi rahisi kuwaelewa wengine. Kama umejielewa kunamaeneo upo vizuri katika utendaji na kunamaeneo haupo vizuri katika utendaji basi katika maisha yako utaelewa kwamba kila mtu anaudhaifu maeneo fulani na kwenye maeneo fulani yupo bora. Wakati fulani huwa nafanya maamuzi haya bila kutegemea basi utaelewa kabisa hata mwenzangu hivo hivo, kwahiyo na imani hiyo inakuwa ni rahisi kutekeleza msamaha.
Ikiwa Ibramu alipata haki kwa imani basi Ibrahimu aliamini kwamba Mungu hawezi kushindwa kufanya lolote lile analolitaka. Imani inahitaji utambuzi ili kupata haki ya kutenda lile jambo unalotaka kutenda. Kama unataka kutimiza jambo ukiwa unafahamu mamlaka yako nni rahisi kutimiza jambo kwa imani. Kwa imani sisi tunavikubali vitu alivyoviumba Mungu, Kwa imani sisi tunakubali kwamba Mungu alimtoa mwanae Yesu Kristo ili achukue dhambi ya ulimwengu pale alipobatizwa na Yohana katika mto Yordani walifanya tendo la kikuhani na sisi kwa sasa hatuna dhambi. Kwa imani tunaamini Yesu aliteswa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu na damu ya agano ikamwagika na sisi tukafanyika, kwa imani tunaamini kwambaYesu alikufa baada ya mateso na kufufuka kutoka kwa wafu na sasa yupo hai juu mbinguni. Kwa imani tunaamini kwamba ametubatiza kwa roho mtakatifu na sasa tunafurahia maisha. Imani hii inatupa haki sisi ya kufanyika wana wa Mungu. Kwa imani sasa tunatekeleza upendo wa Mungu kwa sababu tayari hata sisi tumefanyika pendo kwa kuitwa wana wa Mungu na kujazwa Roho ya Mungu.
Imani inakupa wewe haki ya kutaka unachotaka ili mladi tu unijijenga mwenyewe au la unawajenga wengine. Imani hiyo inakufanya uchukue hatu ya kile ambacho unakiamini. Kwa hiyo rafiki yangu kazana kujijenga ndani mwako na kwa kadili ambavyo unajua zaidi ndivyo unapata haki ya kutaka kile kitu, utambuzi wa ndani ni muhimu zaidi.
Na cha mwisho ambacho ni muhimu ni hiki, kila kitu mwanzo wake ni Mungu, na ndiomaana kila wazo huja kwako bila wewe kutambua na kinachofuata ni utayari wa kupokea kile ulichopokea kwa Mungu huku ukimtumainia yeye. Kwa hiyo imani ni kuishi tumaini wakati wa hivi sasa. Katika ndani ya maisha hayo kuna, imani, utayari na matumaini. Hivi vyote hufanya kazi kwa pamoja.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
0 comments:
Post a Comment