Leo usiku, usiku wa Leo, Mungu amenifundisha kitu kikubwa sana.
Amenifundisha namna ambavyo mchakato wa meli inavyotengenezwa na mwisho kuingia baharini kufanya kazi.
Ukweli ni kwamba, meli hutengenezwa pembeni mwa bahari, (nchi kavu) kwaajili ya matumizi ya baharini.
Katika maisha tumekuwa tunatumia muda mwingi kwaajili ya kusoma vitabu na kujipatia maarifa katika nchi kavu. Ndio, kuna wakati wa utafiti na wakati wa kutendea kazi utafiti.
Inawezekana kwamba Mungu alikuwa ananikumbusha kuwa huu ni wakati wa kung'oa nanga kwaajili ya kutumia yale ambayo nimejifunza.
Meli kuelea juu ya maji ni mfano wa mtu mwenye maarifa kuwahitaji wasio na maarifa.
Katika maisha tunawahitaji watu ambao hawana hawana maarifa ili kuwapa kile ambacho tayari sisi tunacho. Utofauti ndio kitu ambacho tunahitaji ili kuwa watu ambao tunakamirisha utofauti.
Inawezekana umejifunza sana maarifa juu ya sehemu fulani uliyochagua kuishi, basi, huu ni wakati wa kung'oa nanga ili kuanza kazi.
Inuka sasa kwaajili ya kazi, usiwe mtu wa kutengeneza meli daima katika nchi kavu, mtu ambaye usiyetaka kukamirisha kazi yako.
Huu ni wakati wa kung'oa nanga yako. Umewekeza muda mrefu katika kutafuta maarifa, sasa wekeza katika utendaji.
Yawezekana kabisa hata mimi nilikuwa natafiti, na, ndioma Mungu ameamuru ning'oe nanga kwaajili ya kutendea kazi kile ambacho nimejifunza.
Je! Mkulima atafunua madongoa daima? La, akisha kufunua madongoa hupanda mbegu; Nazo mbegu huota, na baadae huzarisha matunda mengi.
Je! Watu hupika chakula na kukiweka katika poti kikae humo daima? La, Wakati ukifika hupakuliwa kwaajili ya kuliwa.
Itupe meli yako baharini, kwaajili ya matumizi yanayopaswa kutumiwa.
Sadick Lazaro Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
0687000768
0 comments:
Post a Comment