Tunapaswa kuishi maisha ya kuona wema ndani ya ubaya wakati wote. Hapo tutaanza kufurahia maisha. Panya huchagua kitu bora kabisa kwenye punje ya mhindi na kuacha kile ambacho hakitaki kama kilivo.
Maisha yamejawa kwa mitindo miwili, wema na ubaya, lakini changamoto inakuja pale ambapo unazingatia jambo ambalo hupaswi kulizingatia. Yafaa tujifunze kutoka kwa panya, tusipoteze muda wetu kwa kuangalia wema na ubaya badala yake ni vema tukajikita katika kuangalia wema nauzuri peke.
Ikiwa utalikataa baya lakini bado unalizingatia ni wazi kwamba utapokea maumivu ya kuzingatia jambo lisilofaa.
Mithali 30:33, Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira huleta ugomvi.
Ikiwa utalibonyezabonyeza puto, hata kama huna lengo la kupasua basi ni wazi kwamba utalipasua kwa sababu unalisukasuka hovyo. Usipende kuzingatia ubaya ndani mwako, usishindane na ubaya bali upuuzie ubaya kwa kuupinga tu. Na unaupinga ubaya kwa kuzingatia mambo mema, hivyo ndivyo tunavyoshinda ubaya na kuona jema kwenye kila jambo.
Kazana kuishi maisha yenye maana na kuzingatia mambo mazuri katika maisha yako, tayari unacho cha kuanzi na uanze na ulichonacho ili kuapa vingine zaidi.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blospot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65gmail.com.
0 comments:
Post a Comment