Kila sehemu katika dunia tunayoishi ni kama muujiza, chochote ambacho unakiona kwa macho ni muujiza kwako. Ninaposema muujiza simaanishi ya kwamba ni kitu cha kutisha au ni kitu ambacho hujawahi kukiona, hapana, japo ni kile kitu ambacho unakiona nje lakini ndani huwezi kuona wala kuadhiri.
Kwa mfano, mchezo wa mpira, kwa kawaida mtu anayecheza ndani anakuwa ndani ya mchezo lakini kuna watu ambao wapo kama watazamaji, hawa huwa wanaangalia vizuri zaidi ya mchazaji mwenyewe lakini hawajisikii kama vile wachezaji wanavojisikia ndani, umeona. Kanuni hii nimeipa jina nje, ndani.
Kanuni hii inagusa katika kila eneo la maisha yetu. Na kama utakuwa makini utatatua kila jambo kwa kanuni hii.
Katika eneo la maisha. Tunaamka asubuhi na kuelekea kwenye shughuli zetu, na Mara nyingi tunakuwa ndani ya wakati, tunakuwa kama wachezaji ambao wanacheza, mara nyingi hatuwezi kutazama kila kitu ambacho tunakifanya. Kumbuka tunaishi ndani ya wakati na ndipo ambapo tutafanya vizuri mambo yetu, lakini si kila kitu tutafanya vizuri, kwahiyo ni vema wakati jioni tukashiriki maisha yetu kama watazamaji na si wachezaji tu.
Katika eneo la mazungumzo, kwanza kabisa kama tunavotambua lugha nini? Ni sauti ambazo zimekubaliwa na jamii fulani ili kuwasilisha ujumbe. Sasa changamoto nini, maneno yanatungwa si kitu ambacho kimejiunganisha na hali ya mtu anavojisikia. Kwahiyo maneno nje lakini kuna mchezo ambao unaendelea ndani, kitu kinachoitwa hali ya mtu, namna anavojisikia. Kwahiyo kama unazungumza na unapaswa kuwa makini ili uone zile lugha za mwili kwa sababu maneno hayatoshi kuwasilisha ukweli.
Eneo la kusoma, unapokuwa unasoma kitabu unapaswa kuwa makini sana, unaposoma tunakuwa tunakalili, tunakuwa nje ya mchezo lakini ili ukweli uwe wako unapaswa uwe ndani ya huo ukweli. Kwahiyo ni vema ukisha soma kitabu ukatafakari yale ambayo umeyasoma yawe hali yako na si mshuhudiaji.
Katika ugomvi, ni vema ukawa nje ya ugomvi kuliko kuwa ndani ya ugomvi. Kuwa mtazamaji wa ugomvi na si mchezaji wa ugomvi.
Kanuni hii inatumika kila mahala, jambo la msingi ni hili unapotumia kanuni ya ndani, nje, kwa mambo ya muhimu hakikisha unakuwa ni mchezaji na ni mtazamaji. Na kwenye mambo ya hovyo wapaswa kuwa mtazamaji kwani hayana budi kuwapo, wewe shiriki kama mtazamaji.
Ukawe na tafakari njema, ukiwa nje ya mchezo wa uliyosoma hapa ili uwe ndani ya mchezo.
Karibu katika group letu la SURA YA UKWELI kujifunza zaidi.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment