Sifa kubwa ya wazee ni kwamba wanekula chumvi nyingi sana, lakini pia wamepitia mambo mengi sana ambayo yamekuwa funzo kwao. Wazee ni hazina kubwa sana.
Sifa nyingine kubwa ya wazee ni kwamba wao huishi kwa kuweka vipaumbele. Wao hawafanyi mambo mengi sana, wao huishi kwa kufuata vipaumbele vyao. Kutokana na kufanya mambo mengi sana katika ujana wao na maisha yao ya nyuma kwa ujumla wametambua hawana haja ya kufanya mambo mengi wakati mda wao wa kuishi umebaki mchache, kwahiyo wao huangalia mambo yao ya muhimu tu na kuyafanya.
Mpendwa msomaji, vijana tunaweza kujifunza kutoka kwao sasa, tunaweza kupata data zao za nyuma kwa kuwauliza maswali, lakini pia tunaweza kuanza kuishi kwa kufanya mambo ya muhimu tu, kwa kufuata vipaumbele vyetu. Lazima tufanye mambo machache yanayotupa matokeo makubwa kuliko kufanya mambo mengi na tusipate matokeo yoyote.
Mpendwa msomaji, sio wazee wote wamefanikiwa kwa hili, kama wameshindwa kujifunza kutoka katika mapito yao basi mapito yao yamekuwa mapigo kwao. Usipo jifunza kutokana na mapito yako basi yatakuwa hatari kubwa sana kwenye maisha yako.
Vijana wakati tilionao ni sasa ili kujenga maisha bora, tusigeuze mapito yetu kuwa mapigo kwetu. Kanuni ya kuishi maisha yenye mafanikio ni kuishi utoto kwa uzingativu, kuishi ujana kwa kutumia vizuri nguvu zetu na kuishi uzee kwa kuweka vipaumbele. Haya ndio maisha bora yasiyo na kharaha.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot. com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment