Kumbuka shetani ni mwelevu sana, anajua ya kwamba ukiwa katika hali hizo huwezi kutumia fikra zako vizuri.
Leo nataka nikuambie rafiki yangu, usifanye maamuzi yoyote yale ukiwa na hasila. Nyakati hizi ambazo mtu anahasila huwa anajiona ya kwamba ameshushwa chini, halafu yeye mwenyewe huwa anajitaidi kwa kujitegemea mwenyewe anajipandisha kwa nguvu. Hasila maana yake ni kujiona ya kwamba umeshushwa chini halafu kwa kujitegemea mwenyewe ujajitahidi kujipandisha. Hasila ni ubinafsi. Mtu mwenye hasila ni mtu mbinafsi. Ajipandishaye hushushwa.
Sasa mara nyingi ukiwa katika hali hii ni ngumu sana mtu kuwaelewa wengine. Kaini sadaka yake iliposhindwa kupokelewa na Mungu, Kaini alikuwa na hasila sana, Mungu akamwambia Kaini, kwanini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Umeona dhambi ipo, wakati wote dhambi inakusubili ufanye kosa dogo hapo ndipo inapojipenyeza.
Lakini Kaini alishindwa kusikiliza sauti ya Mungu, akamwua ndugu yake.
Yatupasa kuwa makini sana tunapokuwa tumefanya makosa au tunahasila, huwa tunashindwa kujidhibiti wenyewe wakati huu, lakini sababu ya yote haya ni hali ya kuwa na umimi yaani ubinafsi. Kosa dogo kwa ajili ya kujiona umekosewa sana inapelekea kufanya makosa makubwa kabisa kama Kaini alivyoenda kumwua nduguye kwa sababu ya wivu.
Wakati wowote ambao unakuwa na hasila kwanza kabisa lazima utambue hakuna mtu ambaye anaweza kukufanya wewe kuwa na hasila kwa hiyo wewe mwenyewe lazima ujiulize kwanini nipo katika hali hii, nimetafsiri vipi hii kauli au kitu hiki nilichokiona, ukiona unaona umekosewa tambua hiyo ni hali ya ubinafsi lakini ukiona unachukulia hilo kama funzo basi wewe ni mshindi. Kumbuka rafiki yangu dhambi ipo ndani yako imelala, inasubiri mtu wa kumwasha na lazima utambue hakuna mtu mwenye mwili ambaye hana kitu hiki kwahiyo wanao tambua kwamba miili yetu imejaa tamaa na ubinafsi hawawezi kufanya kosa hili na hata kama wakikosea basi hujitambua mapema.
Mpendwa msomaji, wewe ni mtu wa hasila basi nakupa mbinu hii hapa, tambua ya kwamba hakuna mtu mbaya duniani ila kuna mabaya. Ukiwa na mtazamo huu utakufanya usimchukie mtu na uchukie hali iliyopo pale. Hasila hupelekea kufanya dhambi zaidi ya dhambi, zaidi na zaidi. Kwa jinsi unavojiona unafaa zaidi ndivyo ambavyo unazidi kufanya makosa zaidi kwa hiyo wakati kama huu lazima ujifunze kujishusha.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment