Katika maisha chochote ambacho utasikia au kuangalia ukweli ni kwamba hakiwezi kukuacha salama. Unaweza kufanya kitu kidogo tu lakini ubongo wako hauachi kunasa sauti au picha ya kitu hicho.
Kuna vitu vitatu ambavyo vinaweza kuharibu maisha yako kabisa, ambavyo ni kuona kitu ambacho hukupaswa kuona, kusema kitu ambacho hukupaswa kusema na kisikia kitu ambacho hukupaswa kusikia. Kwa hiyo rafiki yangu angalia ni kitu gani ambacho unakipa muda sana maana hicho hakiwezi kukuacha kama ulivo kuwa.
Kama unatembea na walevi inamaana hata kama wewe sio mlevi huwezi kuachwa salama, lazima na wewe utakuwa mlevi tu.
Kama utatembea na watu wazuri basi huwezi kuachwa kama ulivo lazima watakuambukiza uzuri wao wa tabia zao.
Ukitembelea mitandao ya internet, huwezi huwezi, kuachwa kama ulivo lazima sehemu ya maisha yako itaathiliwa, kwahiyo ni muhimu kutambua ni mitandao ipi ambayo unatembelea ya kujenga au kubomoa.
Huwezi, huwezi kuachwa kama ulivo katika dunia hii ya matokeo, kila siku kuna vitu vinaingia vipya kwenye ubongo wetu haijarishi unataka au hutaki, ubongo kazi yake ni kunasa tu, kinachoonekana, kinachosikika na kuhisiwa pia.
Huwezi kuachwa salama, muhimu ni kutambua tu mazingira yako, kumbuka ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi, ukitembea na watu wabaya na wewe utakuwa mbaya, kwanini? Kwa sababu kila mtu anamabaya ndani yake yanasubili kuamshwa tu, yakipata mtu wa kuamsha yanaamka.
Endelea kitembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment