Ni siku nyingine tena mpendwa msomaji wa blogu hii ya JIKO LA USHAURI, natumai umeamka salama. Hongera kwa ushindi mkubwa ambao mimi na wewe msomaji wangu tumeshindiwa. Kuiona siku hii mpya ni ushindi mkubwa sana, wapo ambao walikuwa watamani kuiona siku hii lakini hawajaiona, wapo ambao waliiwekea malengo siku hii lakini hawajaifikia, kwahiyo haijarishi wewe upo katika hali gani wewe ni mshindi mkubwa na unaweza kufanya lolote siku hii ya leo na ukabadili kabisa historia ya maisha yako. Hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetushindia.
Majaribu katika maisha yetu ni sehemu ya maisha yetu. Majaribu katika maisha yetu hayana budi kuwepo kwa sababu ni sehemu ya maisha. Adui yetu shetani ataendelea kutunyatia nyatia ili aweze kutunasa na kutupeleka katika maovu yake.
Ukisoma kwenye Biblia (Luka 4:1-13), 1.Na Yesu, hali amejaa roho mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na roho muda wa siku arobaini nyikani, 2.akijaribiwa na ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu, na hata zilipotimia, aliona njaa. 3.Ibilisi akamwambia, ikiwa ndiwe mwana wa Mungu, liambie jiwe hili ligeuke mkate. 4.Yesu akamjibu, imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. 5.Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6.Ibilisi akamwambia, nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo. 7.Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. 8.Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, msujudie Bwana Mungu wako, mwabudu yeye pekee. 9.Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, basi jitupe chini, 10.kwa maana imeandikwa, atakuagizia malaika zake wakulinde, 11.na ya kwamba, mikononi mwao watakichukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12.Yesu akajibu akamwambia, imenenwa usimjaribu Bwana Mungu wako. 13.Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaendazake kwa muda.
Ukisoma mstari huo wa pili utagundua ya kwamba, Ibilisi alikuwa anamjaribu hata kabla ya kujitokeza, akijaribiwa na Ibilisi, na ukisoma mstari wa nne, Yesu anamwambia Ibilisi, mtu hata ishi kwa mkate tu, kwa maneno haya tunajifunza ya kwamba majaribu lazima yawepo na hatuwezi kuishi kwa kutegemea mkate wa kula mda wote kwa hiyo lazima tupitie hali mbalimbali. Lakini pia ukisoma mstari wa kumi na tatu, Ibilisi alienda kwa muda, kwa sababu hiyo lazima atarudi tena. Atarudi tena kujaribu bahati yake kwa sababu yeye huwa hakati tamaa.
Mpendwa msomaji, kesheni maana hatujui siku hata saa ambapo mjaribu wetu atakuja, maana yeye ni mwerevu na hutumia fursa vizuri sana. Wakati wa magumu, Ibilisi huja kukukatisha tamaa, wakati wa ushindi, Ibilisi huja kukujaza tamaa zaidi, wakati wote kwake ni fursa kwa kwahiyo lazima tukeshe vema kabisa.
Majaribu hayana budi kuja kukujenga ama kukubomoa kabisa, jiandae rafiki yangu kwa lolote lile katika kuifikia ndoto yako, mjaribu wako ni mwerevu sana.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment