Tunaweza kujifunza kupitia vitabu hivi, waliona tofauti jambo moja, na hiki ndio kipawa cha mtu. Tunaona tofauti, tunasikia tofauti na kuwasirisha tofauti. tunawasirisha uhalisia uliopo ndani mwetu sio kuongozwa na wengine.
Watu wengi zama hizi tumefungwa na wengine, tumekuwa tukifuata uelewa wa wengine na kushindwa kutumia uwezo wetu uliopo ndani mwetu. Mpendwa msomaji, kila mmoja anakipawa chake, tukijiamini na kuacha kufuata mikumbo lazima tutainua vipawa vyetu, tumeumbwa tukiwa na uwezo mkubwa sana lazima tuwasilishe ukweli wetu na uhalisi wetu.
Watu wengi wameshindwa kuwasirisha ukweli wao kwa sababu wanahisi wao hawafai, wanaogopa kukosolewa, wanajilinganisha na wengine, mwisho wanaona kwamba hawana uwezo wa kutoa maoni yao kutoka ndani mwao. Mpendwa msomaji, kilicho ndani mwako ni kikubwa sana, Mwenyezi Mungu kakujalia hicho lazima ukiwasilishe kwa watu ili ulete ubora wa utofauti kama kwenye vitabu vya injiri. Waliandika kitu kimoja lakini kila mtu aliwasilisha kutokana na uwezo wake. Leo hii vitabu vyote ni vya muhimu japo ni historia moja, aliposhindwa kukazia mwingine vizuri, mwingine alionyesha vizuri na kazi ikaeleweka.
Mpendwa msomaji, imeandikwa alaaniwe tule amutemeaye mwanadamu kwenye biblia, hii ilikuwa inamaana kila mtu kampa uwezo wake lazima tutumie akili zetu vizuri, uzuri ni kwamba akili zetu zinakua yaani tulivyo hivi tumekamilika kinachohitajika ni kuamsha akili zilizolala na kuzitumia vizuri kadili unavyotumika ndivyo nayo inaamka zaidi.
Mpendwa msomaji, tupo duniani kuwasilisha tulicho nacho, dunia inamaswali juu yetu lazima tuyajibu kupitia akili zetu, watu wanatutegemea lazima tutumie vizuri akili zetu, sisi ni zaidi ya tulivo sasa, wewe ni zaidi ya ulivo sasa, tumia akili yako vizuri kujisaidia mwenyewe na wengine pia, acha kumtegemea binadamu mwenzio, tunaona tofauti, tunasikia tofauti na lazima tuwasilishe tulichoona na hapa tutakuwa tinajitendea haki wenyewe. Wewe ni mshindi, umezaliwa kushinda.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment