Karibu katika makala ya leo ambayo mimi nimekuandalia ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja.
Furaha ni kitu ambacho kimekuwa kikitafutwa kwa gharama kubwa. Furaha imekuwa ikitafutwa kwa gharama kubwa kwa kutambua au kutokutambua, lakini mara zote imekuwa ikitafutwa furaha.
Shughuli zote ambazo zimekuwa zikitendeka chini ya jua, kinachotafutwa ni furaha, unaoa au kuolewa ili upate furaha, unatafuta pesa ili upate furaha, unaenda shule ufaulu vizuri ili upate furaha, unaona kitu ambacho unacho na unakipenda na unapata furaha. Kwahiyo shughuli zote ambazo zinafanyika chini ya jua tunachotafuta ni furaha.
Kuna kitu kimoja ambacho kimekuwa kikiwanyima watu kupata furaha, kitu hicho ni, kutaka. Kutaka kumekuwa sababu kubwa ya watu kukosa furaha. Mpendwa msomaji wangu, maisha ni kutiririka kama maji ya mto. Unapokuwa unataka kitu kwa nguvu ndipo mwenyewe unapojinyima furaha yako.
Mpendwa msomaji ndio maana katika maisha unapaswa kuwa mhusika mwenyewe na uwe mtendaji mkuu. Kuna kitu kikubwa sana ambacho watu hawakitambui, unachokitaka sicho ambacho kitakupa furaha, kumbuka unapotaka kitu, unashindwa kutiririka kuna nafasi fulani unairuka na hapo ndipo kwenye tamaa na furaha yako itakuondoka. Ukitamani kitu lazima utambue miongozo ambayo itakupelekea kupata kile ambacho unakitamani.
Matendo ni muhimu sana katika safari ya kuipata furaha. Furaha ipo na itaendelea kuwepo, huta ipata baada ya kupata kitu furaha na kamwe kama unategemea hivi huwezi kufurahia maisha. Tiririka kama maji ya mto nawe utajazwa furaha.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi. OMBI: nisaidie kuwashirikisha ujumbe huu wengine ili upate kuwasaidia wengi zaidi. Maoni yako ni ya muhimu.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment