Mpendwa wangu rafiki yangu karibu sana kwenye makala hii ya leo ambayo mimi rafiki yako nimekuandalia ambapo nitakuonyesha mbinu mbalimbali za kujifunza ili kuongeza maarifa kwenye maisha yako.
Kwanza naomba nikutaarifu ya kwamba sisi watu wa ngozi nyeusi hatupendi kujifunza kabisa yaani mtu kujifunza anaona ni kitu cha ajabu sana yaani tunapenda kila kitu kwetu kiwe rahisi tu kama kuangalia TV maana kuangalia sio kazi ila kazi ipo kwenye kulichukulia lile jambo ambalo umeliangalia yaani wewe binafsi unamutazamo gani juu ya kitu ambacho umekiangalia.
Wakati tulipo hitimu ngazi mbalimbali, tujua tumesha maliza kila kitu lakini ukweli ni kwamba hujamaliza na huwezi maliza kwa sababu mambo yanabadilika sasa kama mambo yanabadilika wewe usipo jifunza si utaachwa pale na mawazo yako ya zamani unaweza ukasema mbona mimi naona poa tu mambo yanaenda, kiuhalisia yanaenda lakini lazima ujue wewe unaendeshwa mara huku mara huku kwa sababu huna upekee uliopo ndani yako. Kwahiyo kujifunza kunakupa wewe upekee wako binafsi.
Sasa nisikuchoshe sana mpendwa wangu ngoja tuende mojakwamoja katika mbinu mbalimbali za kujifunza kwenye maisha.
Mbinu ya kwanza ni kujifunza kupitia mazungumzo yako na mtu mwingine au kikundi fulani. Sasa hapo kila neno linalozungumzwa lazima ulichukulie kwa uzito kiasi na uliangalie kwa mtazamo wako binafsi na ili kujifunza zaidi lazima uwape nafasi zaidi kuriko wewe kuwa mzungumzaji zaidi na wewe unakuwa msikilizaji sana kuriko kuzungumza. Haijarishi yuho mtu anazungumza kitu gani hata kama ni pumba anaongea lazima usikilize itakusaidia kitu fulani. Kama wewe unataka mambo mazuri kila siku sasa mabaya utayajuaje? Kuwa msikilizaji.
Penda sana kujisomea vitabu mbalimbali. Hii mbinu kwangu mimi naichulia kama mbinu kuu katika kujifunza, usomaji wa vitabu una raha yake bwana na hapa ndipo kwenye maarifa ya watu chanya, kwa sababu mtu anayeandika kitabu huwa anatoa kitu kilichopo ndani yake kwahiyo kama wewe ukikisoma kile kitabu tayari unachukua upekee wa mtu mwingine. Sasa ukisoma vitabu vingi utatengeneza kitu kipya kutoka kwenye vitu mbalimbali. Mpiganaji BLUES LEE alijifunza style mbalimbali za mapigano halafu akaja kutengeneza kitu ambacho kipya kabisa na ndicho kilicho mpa jina kubwa.
Jifunze kupitia internet. Saizi mambo yamerahizishwa yaani mda wote unaweza kujifunza yaani kila kitu kipo poa tu unacho taka unakipata.
Jifunze kupitia mikanda mbalimbali ya cd. Ndio unaweza kujifunza kupitia mbinu hii kwa kuangali tv ukajifunza.
Zipo mbinu mbalimbali za kujifunza ni nyingi sana kama luenda kwenye semina kwahiyo ni nyingi sana lakini kujifunza ni jukumu lako wewe lazima uongeze maarifa kwa namna yoyote ile na kujifunza ndiko kunawapa watu mafanikio pia kunawapa watu uhuru wa maisha.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment