Kiasili vitu nyote vya dunia vipo katika hali ya upacha au uwili. Uwili huu upo katika kila kitu hapa duniani. Kuna uwongo na ukweli, mrefu na mfupi, mnene na mwembamba, mbali na jilani, kutaka na kutotaka, na mengine mengi yapo katika hali ya upacha.
Upacha huu una kazi moja kubwa, ni kutofautisha kati ya moja na nyingine, mfano unaweza kusema huyu ni mnene na huyu ni mwembamba, kule ni jilani na kule ni mbali.
Mashindano mengi katika dunia hii yanatokea kutokana na upacha huu, ukweli ni kwamba upacha huu ukianza kutumika kama mashindano huibui mambo mengine ya tofauti. Mungu aliuweka upacha au utofauti huu ili kuweka ubora tu. Mashindano mengi yanatokea kwa sababu ya utofauti, lakini wengi huwa tunasahau ya kwamba kila kitu kina ubora wake.
Mtu anaweza kuibua jambo ambalo si kweli, lauongo kabisa akalipeleka katika hali ya ukweli, akaaminisha watu kuwa jambo fulani ni kweli na wengine wakapokea kama ni kweli lakini bado kunawengine wakasimamia katika ukweli halisia. Mambo haya yanatokea sana katika jamii, kwamba mtu anaibua jambo kwa tamaa zake na kuwadanganya watu na kulipeleka katika hali ya ukweli kumbe si kweli, yeye anatafuta matakwa yake tu.
Hofu nyingi katika maisha ya watu zinatokea katika hali hii hii ya utofauti wa upacha huu, tunaona ya kwamba wanaume sasa wanataka kuwa wanawake kitu ambacho hakiwezekani kabisa, wanawake weusi wanajikana wenyewe na kutaka kuwa weupe, mwanamke mweupe akijiunua na kusema mimi ni mzuri kuliko mweusi, mjinga mweusi anajiona kana kwamba yeye hafai kabisa na ndipo anaanza kujichubua na kuondoa asili yake ya zamani na kuweka ya kwake yote haya ni kwa sababu ya upacha wa utofauti.
Matumizi mabaya ya upacha huu huleta madhara makubwa sana katika jamii, lazima tutumie vizuri utofauti wetu ili kujenga ubora zaidi na tufanye dunia ni mahali salama, kubali mazingira yanayokuzunguka, kuwa jasili, kila kitu kina sababu zake.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment