Mienendo yako lazima ikuhakikishie ya kwamba inakuweka salama, tabia yako lazima ikufanye uwe salama, huwezi kuwa salama kama unatabia mbaya ya kuwa na wapenzi wengi, kugombana na watu, ni mtu wa kuvunja sheria za barabarani, mwizi, utapeli, na mengine mengi ambayo ni hatari kwa wengine.
Wakati wowote jihakikishie upo salama, fanya kila kitu ambacho cha usalama kwako na kwa wengine pia, mdomo wako ni kitu hatari sana katika jamii, ulimi unaweza kubomoa au kujenga, wakati wowote jiulize maneno yangu yanawafanya watu kuwa salama, ukweli ni kwamba watu wakiwa hawana usalama na wewe pia hupo salama kabisa.
Mpendwa msomaji, furaha unayoitafuta huwezi kuipata kama haupo salama, afya yako lazima iwe salama, kula kwa afya, kula kwa mpangilio, fanya mazoezi, fanya sala kuupa mwili nguvu, pata muda mzuri kabisa wa mapumziko, angalia mazingira uliyopo je yanakuweka salama kiafya? Kuwa salama siku zote.
Kuwa salama kiakili, watu gani ambao unawapa muda mwingi kimahusiano? mitandao ipi ya kijamii unayotembelea? Je unafanya nini ili kuijenga akili yako? Kuwa salama kiakili, akili yako ndo kila kitu, marafiki wanaweza kujenga au kubomoa akili yako, na mitandao ya kijamii pia hatari kwenye akili zetu. Pata muda wa kutafakari juu yako mwenyewe na maisha yako ili utumie akili yako vizuri.
Jihakikishie usalama rafiki yangu, usipo kuwa salama utakosa furaha na utashindwa kuzifikia ndoto zako, maisha yako yatakuwa magumu. Usalama wa maisha yako upo juu yako, kikubwa kuacha tabia mbaya zote ili kujihakikishia usalama.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment