Ni kawaida kwa watu, tunapo pitia katika changamoto zetu kulalamika na kuwa na lawama nyingi sana. Tunapopitia katika changamoto huwa lazima minung'uniko itasikika. Misemo mbalimbali itaanzishwa na watu ili tu, kuonyesha ya kwamba tunapitia hali ngumu. Misemo kama vyuma vimebana, hali ngumu na lugha za malalamishi kwa watu kuonyesha tunapitia katika changamoto.
Wengine huimba nyimbo hizo hali wakiwa nyumbani tu na kusema, hali ngumu. Kwa bahati mbaya ni kwamba hata ukiimba kwa nguvu vipi kama wewe binafsi huta kuwa na makusudi ya kuchukua hatua ili kufanya vyuma vilegee, huo utakuwa wimbo wako wa kila siku. Maisha hayakusikii wala hayakuelewi, mambo yanakwenda mbele.
Mpendwa msomaji, ni wakati wa kuacha kulalamika sana, ni wakati sasa wakutumia maamuzi zaidi na sio malalamishi. Ukiona mambo hayapo vizuri, tafuta njia ya kuondoka hapo penye ugumu. Weka kazi na sio kulalamika sana. Kwa chochote unachopitia tafuta suluhu na sio kulalamika.
Mara nyingi sana watu tunalalamika kwa sababu tunahisi ya kwamba sisi hatuhusiki katika jambo hilo. Tunawapa lawama wengine na kusema wao ndio wamesababisha na kutufikisha hapo tulipofika, lakini ukweli haupo hivo kabisa, tupo tulipo kwa sababu ya hatua tulizo chukua huko nyuma. Mpendwa msomaji, tatua matizo yako acha kupiga kelele, na kulalamika, maisha hayakusikii yenyewe yanasonga mbele.
Tuache kuwa walalamishi sana katika hali mbalimbali tunazopitia, mbona mambo yakiwa mazuri tupo kimya? Basi vivo hivyo na tuwe katika hali ngumu tuwe kimya.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi. Maoni yako ni muhimu.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushairi.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment