Rafiki yangu dunia hii imejaa giza nene sana si mchana si usiku bali kuna giza nene sana na ndio maana mara nyingi tunajikwaa katika changamoto mbalimbali. Giza hili nene kuna mambo ambayo limeficha rafiki yangu sasa ni wajibu mimi na wewe rafiki yangu kufichua hayo mambo. Na kila mmoja katika giza hili anawajibu wake na nafasi yake ya kuangaza katika sehemu ambayo yupo.
Wakati unatoa kile kitu ambacho kimejificha ndani yako basi hapo unaondoa giza ambalo limejificha ndani yako na hiyo ndio dunia yako. Wakati unaangaza na kutoa mwanga kwa wengine kwa kutoa huduma ya kipekee basi hapo umeleta mwangaza kwa wengine na wewe unakuwa unang'aa. Inasemekana kuwa nyota unazoziona kule juu wale ni binadamu.
Giza unaloliona angani na unaona nyota inaangaza katika nafasi yake hivyo ndivyo maisha yalivyo kwahiyo dunia imejaa giza lakini kila mmoja anaangaza kwa nafasi yake. Rafiki yangu angalia kwa umakini namna nyota zilivo jipanga na kisha jitadhimini wewe ni nani katika hizo nyota nyota iliyo fifia au nyota inayo ng'aa? Giza lile ni jamii, jamii inakuhitaji wewe uangaze kwa nafasi uliyopo na kama hutoangaza kwa nafasi yako giza litatanda.
Rafiki yangu wewe upo kwenye dunia kwaajili ya wengine acha kuwa mbinafsi kilicho ndani yako wape wengine wanufaike. Ukweli ni kwamba hakuna rangi nyeusi wala nyeupe ila ni kwamba penye weusi [giza] panahitaji weupe [mwanga] ili pawe peupe na ndio maana huwezi kuwasha taa wakati wa mchana.
Washa taa kwenye giza yako watu wanahitaji mwanga wako. Endelea kutembelea blogu hii ya JIKO LA USHAURI ili kujifunza zaidi.
Kanuni ya maisha ni KUWA+FANYA=POKEA.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 068700768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment