Mpendwa rafiki yangu kati ya kipindi ambacho mambo yote yapo sawa basi zama hizi mambo yote yapo tayari, ni kila nyanja mambo yapo sawa na tunainjoi sana kuishi zama hizi ambazo ni zama za mawasiliano. Chochote unachotaka kipo tayari ni wewe kukamirisha tu ratiba yako, kitu gani unataka? puliza kipyenga sasa.
Je unataka kuanza biashara na hauna mtaji? Huwezi kusema siwezi kuanza biashara kwa sabababu sina mtaji wa kuanzia utakua unakosea sana japo hukosei kwa namna moja au nyingine unakosea, zipo biashara ambazo unaweza kuanza hivyohivyo ulivyo na ukaendelea mbele. Biashara kama network marketing[biashara ya mtandao] ni biashara ambazo unawza kuanza bila ha mtaji.
Je unataka kuanza mazoezi na unashindwa namna ya kunza? Tayari kila kitu kipo cha kukuongoza ni wewe tu sasa kusema sasa nataka kuanza mazoezi download alamu aplication ambazo zitakuamsha asubuhina jifunze namna kuanza mazoezi, zipo aplication ambazo zina sound ambazo zitakupa hamasa ya kuendelea kufanya mazoezi.
Unataka kuandika na kuacha alama kwenye maisha yako kila kitu kipo sawa, blogu ni jukwaa zuri sana la kuandika na unakuwa unaandika mafunzo au habari yoyote ile unayotaka kutoa cha msingi uwe unatoa kitu cha dhamani kwenye jamii na inafaidika kutoka kwako na hapa ndipo unapoweza kuanza kutengeneza kipato chako kwa kutumia tu simu hiyohiyo uliyo nayo, kwahiyo tayari biashara bila mtaji.
Je wewe unataka marafiki wa ukweli wa kusafiri nao katika ndoto yako unaona kama huna watu sahihi? Mpendwa wangu kama wewe upo tayari basi wapo wengine nao wapo hivohivo sasa wewe anza kuwaonesha watu hao ya kwamba wewe ni mtu sahihi sasa kama hivi kama wewe unataka kwa rafiki yangu au mtu wangu wa nguvu basi jaza form hapo chini tayari unakuwa rafiki yangu tutakuwa wote.
Kila kitu kipo sawa ila wewe haupo sawa na wewe ndio refa wa maisha yako, na kila kitu kina mda wake kama ulivyo mpira wa miguu ni dakika tisini tu kwahiyo ndio maana tuliwekewa masaa, kama huchukui hatua shauri yako. Mchezo dakika tisini tu unaweza ukaishi kwa mfumo huo tu kwa kuchukulia maisha yapo ndani ya dakika tisini, ukipoteza dakika moja inakula kwako.
Puliza kipyenga sasa wakati ni sasa hili ndilo jambo la msingi kwenye maisha yako na chukua hatua.
Fanya kazi kwa ugumu utafanikiwa.
Wako SADICK KILASI
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com
0 comments:
Post a Comment