Kitu chochote ambacho unakazana kufanya ndicho ambacho kitainuka na kuwa kikubwa sana. Jambo lolote lile ambalo unalipa kipaumbele sana litajengeka na kuwa kubwa sana.
Je wewe unanjaa na kiu ya kitu gani? Unafanya nini? Au unagusagusa tu mambo yako, Leo unafanya hiki, unaacha, kesho kile, unaacha, kesho kile, unaacha, hijaweka vipaumbele, utajazwa kwenye nini?
Chagua kitu kimoja ambacho unapaswa kukijengea misingi na kusimamisha kwa uhodari na ni jambo ambalo ndilo litakuwa legasi katika maisha yako. Jambo ambalo hata kizazi kijacho kitasema hii ni kazi ya mtu fulani, tunajivunia kwa kazi yake nzuri.
Tengeneza misingi, tengeneza uhodari, usiwe mtu wa kufanya kila kitu lazima uwe na njaa na kiu ya haki, Mwenyezi Mungu katuahidi kutujaza. Lazima uwe hodari katika mapito yako, Mungu alimwambia Joshua uwe hodari, kuwa mkakamavu utashinda.
Njaa na kiu ya haki, mpendwa msomaji, hali ya uhitaji mkubwa sio kilele mama hapana, lazima uoneshe ushirikiano kweli kweli ndipo utapata unachokitaka. Mpendwa, sio lahisi kutengeneza misingi yako, lazima ufanye kwa bidii na ndipo utapata unachotaka.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment