Adui mkubwa na anaye nyanyasa maisha ya watu ni msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ni vita ambavyo vipo ndani ya watu na wakuvimaliza vita hivyo ni mhusika mwenyewe.
Anayepitia katika hali hii ndiye uwanja wa vita, ndani mwake mnapigana vita ambavyo si vyakawaida. Kuna wakati ambao mhusika huonyesha dhahili kabisa hali anayopitia. Msongo wa mawazo ni utumwa wa fikra.
Kuna chanzo kikuu kimoja cha msongo wa mawazo, mtazamo ndo chanzo kikuu cha msongo wa mawazo. Japokuwa kuna vyanzo vingine vya msongo wa mawazo lakini mtazamo ndo chanzo kikuu cha msongo wa mawazo.
Kukosa pesa inaweza kusababisha msongo wa mawazo lakini kama mhusika ukitambua namna ambavyo pesa inatakiwa hata lalamika ya kwamba sina pesa, wakati kuna mambo mengine ya muhimu yapo salama kama chakula, mavazi na sehemu ya kulala. Mtazamo utakusaidia namna ya kufikia katika hali fulani ya maisha bila ya kuwa na woga wowote wala masumbuko.
Mrundikano wa mawazo unaweza kusababisha msongo wa mawazo lakini kama mtazamo wako upo vizuri inamaana utajua namna ya kupangilia mambo yako muhimu na yasiyo muhimu.
Mtazamo ni uwezo wa kupambanua hali fulani au jambo fulani. Kuna mtazamo mzuri na mtazamo mbaya. Ukiwa na mtazamo wa hovyo kila kitu kwako kitakuwa ni tatizo na hapo ndipo chanzo cha msongo wa mawazo kwahiyo matatizo yote unayoyaona chanzo kikuu ni mtazamo wako.
Tatizo ambalo unaliona ni tatizo kwako kwa mwingine si tatizo. Mpendwa rafiki yangu kuwa tajiri wa mtazamo maisha yako yatakuwa bora kweli kweli. Jifunze kwa mapito yako, soma vitabu na kuwa msikivu.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment