Soma SEHEMU YA KWANZA, kama bado hujasoma uchambuzi huu.
13.Mwili wangu ni kama pipa la taka taka, siwezi kuutegemea mwili. Ninamsifu Mungu wangu kwa moyo wangu, ninamwamini yeye.
14.Ukweli ni kwamba dhambi tunazofanya ni nyingi sana na hazihesabiki, kama tungekuwa tunafanya dhambi chache basi tungeomba toba na mambo yangeisha. Mungu ameturehemu kwa Kristo Yesu Bwana na Mokozi wetu kwa kutufanya huru siku zote za maisha yetu.
15.Hakuna kitu cha kukitegemea katika mwili vyote hivi vina ukomo lakini kwa Bwana kuna umilele tu. Lazima tutafute kitu ambacho ni cha milele.
16.Mioyo yetu siku zote inamtumikia Mungu lakini miili yetu siku zote hutenda dhambi siku zote kwa sheria ya dhambi. Bwana wetu amefutilia mbali dhambi zetu za zamani, sasa na baadae. Miili yetu haita acha kufuata dhambi. Tunamshukuru Mungu kwa hili ambalo haliwezi hata kuelezeka. Mwili hutumikia sheria ya dhambi.(warumi 7:24-25).
17. Watu ambao wanamtumikia Mungu hukosa furaha pale ambapo huhisi ya kwamba wametenda dhambi na tusije tukafikiri ya kwamba hatuwezi kutenda dhambi kamwe ili tuwe na furaha. Lakini ukweli ni kuwa hatuna ujasiri wa kuwa hatuta tenda dhambi kamwe au kabisa.
18.Tunaweza kumtumikia Mungu kwa kitambo kidogo tu kwa hamasa lakini hamasa hiyo huisha pale tu mwili unapotenda dhambi, hapa udhaifu huanza tena. Mwili hufuata dhambi na hii ni sheria ya dhambi. Ndo maana mtume Paulo anatenga mwili na roho. (warumi 7:24-25).
19.Usitegemee mengi kutoka katika mwili.
20.Mwili unapenda kukuza raha ya mwili, starehe, amani, furaha na majivuno yake na si haki ya Mungu. Mwili unapenda vitu vyote vifanyike kama unavopenda. Mara nyingi mwili unapenda kujihesabia haki wenyewe. Hebu tuache kujihesabia haki wenyewe na tuuache mwili kama ulivo.
21.Tunaweza kufurahia maisha wakati wote ikiwa tutambua ya kwamba dhambi zetu zote zilikombolewa na kusamehewa, tukiokoka tunapaswa kutenda mema lakini mwili wetu huu wa mauti utaendelea kuishia katika dhambi. Basi tunapaswa kuomba toba, tusiishi kama watu wa kujitegemea wenyewe kwamba tukitenda dhambi tutaipoteza furaha yetu, hapana lazima tufurahie maisha.
22.Ikiwa tutatambua ya kwamba mwili wetu unatumikia sheria ya dhambi tu, basi tunaweza kukwepa dhambi kwa imani. Tukiishi kuamini kwa imani kwamba Bwana alituokoa dhambi zetu zote basi na tujengeke katika Neno lake. Hata kama tunatambua ya kwamba tunaweza kutenda dhambi tena lakini tunaamini kwa imani kwamba dhambi zetu zote zilikombolewa na Kristo Yesu na tudumu katika Neno.
Kwa leo ninafikia hapa mpendwa msomaji. Hongera kwa kuwa pamoja na katika mwendelezo huu wa uchambuzi. Ombi langu kwako wewe msomaji kutafakari mambo haya ninayo kushirikisha. Kama bado hujasoma sehemu ya kwanza basi hakikisha unaisoma, tafuta katika tafuta blogu hii utaipata.
Mtu hawezi kujengeka kama hakuna kitu ambacho kinamsukuma aweze kujengeka, mfanya nazoezi anajengeka kimwili kwa sababu ya mazoezi yake, wewe utajengeka kiakili kwa sababu ya kusoma na kutafakari. Maoni yako muhimu, toa maoni au nitumie meseji katika Mawasiliano yangu nitakujibu.
Nikutakie tafakari njema katika haya, tukutane tena katika mwendelezo ujao. Washirikishe wengine ujumbe huu uwasaidie wengi zaidi. Mungu awe nawe.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment