Sasa waweza kujiuliza ya kwamba sasa inamaana gani kama nikiwa tajiri sifurahii utajitari wangu na nikiwa maskini nakosa furaha. Mpendwa msomaji kuna sababu ambazo huwa zinapelekea kukosa furaha hii, sio kila tajiri hana furaha na siyo kila maskini hana furaha. UBINAFSI ndicho kitu ambacho hupelekea matajiri na maskini kukosa furaha.
Kwa hali ya kawaida ni kwamba ubinafsi hauchagui wa kutawala maskini na matajiri, ubinafsi ni pale ambapo unashindwa kujiweka nafasi ya wengine. Kwa kawaida ubinafsi unaumiza zaidi hata kuliko matatizo tuliyo nayo. Ukiwa na pesa na ukawa mbinafsi utateseka, ukiwa maskini na ukawa mbinafsi, ahaa wewe ndo kabisa maana utakuwa na kibuli cha kutosha, maisha yako yatakuwa magumu sana.
Hivi ushawahi kusikia hasa kwa maskini anakwambia, natafuta hela ya kula tu, katika maisha ukijikuta kila siku unatafuta, kwaajili ya mahitaji yako basi ni hatari sana, maisha yatakuwa magumu, unachokazana wewe ni kutatua matatizo yako binafsi na unashindwa kuangalia wengine na kusema natafuta hela ya kula tu. Mpendwa msomaji, tumezaliwa kuwasilisha tulicho nacho kwa wengine, kama sivyo haja ya kuzaliwa isingekuwepo kabisa. Tumezaliwa kutumika kwa wengine.
Kama wewe unafikiri kukusanya vitu vya dunia hii ndio utamaliza matatizo yako basi unafeli, utajiri sio wa pekee yako, umebarikiwa kuwa baraka kwa wengine. Kuwa na pesa sio njia ya kuwaonyesha watu kwamba wewe unazo lazima utakuwa na maisha magumu sana, kuna vitu ambavyo pesa hawezi kununua, utu wa mtu, na kama unaona ya kwamba mbona nawanyanyasa basi unawanyanyasa wenye tamaa kama wewe.
Kama wewe maskini unafikiri huna haja ya kufanikiwa basi wajipotodha mwenyewe, ukiushinda ubinafsi mafanikio kwako ni kitu rahisi sana na yatakufuata yenyewe. Kocha Makirita Amani anausemi wake unaosema, Mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa ni wewe tu uamue ufanikiwe au usifanikiwe. Sasa kama wewe ni mwenye uamuzi, uteseke na ubinafsi wako maana kushindwa kufanikiwa pia ni ubinafsi, kuna kitu ambapo umeshindwa kuipa jamii na ndio maana umeshindwa kufanikiwa. Tajiri jali utu kuliko vitu na maskini hivo hivo.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment