Wakati tulipo zaliwa, tulizaliwa tukiwa tayari na tunapaswa kuenenda katika uhalisia wa asili ambao Mwenyezi Mungu alituandalia. Tulipaswa kutiririka kama maji ya mto katika safari yetu ya maisha. Ukivunja sheria ya asili ya dunia lazima utapewa adhabu. Yusuph aliyeandikwa katika kitabu cha biblia, alivunja sheria kwa kuwaambia ndugu zake habari za maisha yake na namna ndugu watakavo msujudia ilibidi apewe adhabu kwa kuuzwa na ndugu zake hao hao alio wambia ambao walikuwa hawana uwezo wa kuvumulia. Mungu alimwonesha maisha ya baadae lakini yeye akawaambia ndugu zake ikabidi apawe adhabu.
Mpendwa msomaji, kama unapitia changamoto kwa sasa, tambua ya kwamba unapitia katika adhabu yako, kuna sehemu umevunja sheria kidogo ndiomaana unaadhibiwa. Mungu anataka utambue makosa yako mwenyewe ili utoke katika adhabu yako. Ndio maana si vizuri mtu anayepitia wakati mgumu kumsaidia ni vizuri yeye mwenyewe kujisaidia ili afikilie vizuri wapi alikosea? Na awe na majibu sahihi ili baadae isiwe changamoto tena kwake.
Je unapitia katika changamoto nzito? Basi yakupasa utubu makosa yako ili uanze tena, dunia haiwezi kukuacha ukawa unakosea na kutafuta mbinu zako za maisha lazima uadhibiwe. Ukishindwa kuchagua mwanamke mzuri wa kukufiti dunia lazima ikuadhibu, ukitafuta utajiri wa haraka dunia lazima ukuadhibu, haiwezi kukuacha salama katika mapito yako ya kuvunja sheria.
Lakini pamoja na adhabu unayopitia nikutie moyo ya kwamba ukitubu, furahia ukiwa katika adhabu hiyo maana ikitoka hapo si sawa na ambaye hajakosea, si sawa na ambaye hajapitia katika adhabu hiyo, utakuwa mkomavu haswa, huta tikiswa na hutatikisika kwa kitu rĂ¡pido. Upitiapo changamoto jifunze na ufurahi maana kwako ndio mwanzo wako wa ushindi.
Sheria ya asili ya dunia inakuadhibu ukishindwa kuifuata, huwezi kuachwa hivi hivi ukitafuta mbinu zako na kuvunja sheria lazima utapokea adhabu lazima ujifunze, unapotaka kitu bila kufanyia kazi dunia inakuadhibu kwa sheria yake kwa sababu ya tamaa yako. Ishi maisha, acha kutaka, tafuta, usitafute mbinu, tiririka, mbinu zitakuumiza.
Endelea kutembelea blogu hii ili kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment