Karibu mpendwa msomaji tutafakari kwa pamoja hekima hii, ambayo tumeachiwa itusaidie katika maisha yetu.
Kwa kawaida kila binadamu ameumbwa akiwa na uwezo mkubwa sana, kila mtu ameubwa akiwa bora katika maeneo fulani au na katika mambo yale ambayo hayupo bora anauwezo wa kufanya akuwe na awe bora pia. Kwa mfano, wewe unaweza ukawa na kipawa cha uimbaji, kumbuka kipawa ni zawadi ambayo mtu anazaliwa akiwa nacho, lakini pia licha ya kuwa na kipawa cha uimbaji unaweza ukafanya kitu kingine na ukawa bora pia, mfano, unaweza ukawa mkulima mzuri tu kutokana na kujiendeleza mwenyewe.
Kwa kawaida binadamu anamapungufu, na mapungufu huwa yanaonekana ni mengi kwa sababu kama unavojua dunia hii mabaya ndiyo huwa yanasambaa haraka sana. Kuna wakati unaweza ukajikuta kama wewe si lolote si chochote yaani unajiona kana kwamba wewe huwezi kitu, Si bora kwa chochote. Sasa Lincoln anatukumbusha ya kwamba kwa vyovyote vile ulivyo, jitofautishe kwa jambo zuri.
Wewe una jambo zuri unalo, unaweza kuwa unajua, harafu unadharau kwa sababu ya kuambiwa au kukata tamaa na kuona huna jambo zuri ambalo unaweza kufanya na kuipa jamii kitu. Waweza pia ukawa hujui kwamba wewe upo bora maeneo yapi, lakini nakwambia rafiki yangu nikutie moyo tu kwamba wewe ni bora sana, hebu tafuta eneo ambalo ukifanya unaona kwako wewe ni bora au angalia jamii na ona mapungufu yako wapi na uwe na kiu ya kwamba jamii inependeza ingekuwa hivi hivi na hivi.
Mpendwa msomaji, kila mtu ni barua, barua ambayo jamii inahitaji isome, kumbuka tumezaliwa kuijaza dunia sehemu ambazo zinamapungufu, sasa hayo mapungufu uliyo nayo na sehemu ndogo unayoiona ni bora kwako basi hiyo ndiyo sehemu ambayo jamii inahitaji.
Una mengi mazuri ambayo jamii inahitaji kutoka kwako, usione mapungufu mengi kutoka kwako hayo ni sawa na maharage mabovu tu yanayojitokeza haraka lakini kuna mengi mazuri yapo chini anza sasa kutumika katika sehemu ndogo au uzuri ulionao.
Wewe ni tofauti na wengine, tuna vidole vitano kila kidole kinasaizi yake lakini ili ngumi iwe na nguvu vidole vyote vinahitajika na ubora unakuwepo. Wewe ni wa tofauti na wengine, utofauti wako ndiyo kitu pekee ambacho jamii inahitaji ili kutengeneza ubora, tafadhari, tafadhari usiinyime jamii ulichonacho na hapo ndipo mafanikio yalipo.
Endelea kutembelea blogu hii ili kijifunza zaidi.
Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment