Sasa waweza kujiuliza nini chanzo cha yote hayo, lakini ukweli ni kwamba TAMAA ndio chanzo cha matatizo hapa duniani. Kaini alikuwa na tamaa juu ya mazao yake, alikuwa analima anapata vizuri, mazao yanastawi, lakini yeye alikuwa na tamaa akawa anatoa zaka mbovu au matoleo mabaya kwa Mungu. Anachagua vile ambavyo ni vibovu ndivyo anamtolea Mungu.
Matatizo mengi hapa nyumbani Afrika, vita vingi, mauaji mengi yanatokea hii yote ni kwa sababu ya tamaa. Viongozi wanatamaa na uloho wa madaraka. Tunaona nchi nyingi zina vita vya wao kwa wao yote hiyo ni kwa sababu ya tamaa.
Mpendwa msomaji, mtu yeyote yule ukimkuta na mawazo mengi ni kwa sababu ya tamaa. Lazima kuna kitu anataka na hapo ndipo mwanzo wa mawazo ya mtu huyo. Tamaa ndiyo vita ambayo tunapaswa kupigana nayo, tamaa ndio mwanzo wa matatizo yote.
Leo hii vijana wengi wapo mitaani wameharika kwa madawa ya kulevya yote hiyo ni kwa sababu ya tamaa. Waliamani watakuwa matajiri lakini hawakutaka kulipa gharama ndipo wakajiingiza kwenye madawa ya kulenya kwa sababu ya msongo mawazo.
Tamaa huzaa mauti, ukitaka sana mwisho utakuwa takataka. Maisha yanahitaji utulivu, wacha kukuza matatizo na kujiona wewe ndiye mwenye matatizo sana, unataka kila kitu unakazana tu kukusanya tu bila kupunguzwa mwisho utakuja kupasuka. Ndio maana kuna kujumrisha na kutoa, hasi na chanya, zidisha na kugawanya, yote hii imekuja kwetu ili tutambue ya kwamba ukizishiwa kumbuka kugawa, ukiongezewa kumbuka kutoa. Toa zaka hata kama kipato chako ni kidogo au kikubwa, dunia huwa inatabia ya kujaza pale ambapo patupu na kupunguza palipo jaa. Anza kuishinda tamaa kwa kutoa zaka hata kama kipato chako ni kidogo kiasi gani.
Kutoa zaka ni kwaajili ya sisi wenyewe, Mungu kaweka sheria hii ili tuwe na shukrani. Shukrani ni uwezo wa kutambua mazuri juu ya mabaya. Kwa sababu hiyo Mungu kaweka zaka ili sisi tupate kuwa na furaha kwa shukrani.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment