Mpendwa msomaji, kumekuwepo na watu ambao wanasumu kubwa sana ya chuki dhidi ya wengine. Yaani mtu anaishi na chuki kama mafuta ambayo yanasubiliwa kulipuliwa na moto au gesi ambayo inataka kupasuka. Watu wamekuwa na chuki ndani yao, watu wamekuwa wanasumu kali ndani yao, kitu ambacho ni hatari sana kwao na kwa wanao wachukia pia.
Kuna sababu ambazo hupelekea wengine wawachukie wengine. Japokuwa kuna sababu ambazo zipo, isiwe sababu kwako wewe msomaji wangu kuwachukia wengine, wewe ni mwanaharakati wa ukweli na upendo, lazima usimamie ukweli na upendo na usiwe na sababu yoyote ile ya kumchukia mtu. Sasa hizi ni sababu ambazo zinapelekea wengine kuwachukia wengine.
1.Kumwangalia kwa mtazamo wa ubaya tu. Hii ni sababu kubwa sana ambayo inapelekea wengine kuwa na chuki na wengine. Sisi binadamu kwa kawaida tunatabia ya kuangalia mabaya tu kwa wengine lakini hatuwezi kuangalia kwa jicho la uzuri. Mpendwa msomaji, ukiona mtu ni mbaya kwa wengine usimchukie yeye bali chukia mabaya ambayo yapo hapa duniani, chukia macho yako na fikra zako ambazo zinaona mabaya, acha kuhukumu mtu mwingine msome mtu kwa mzuri tu, jicho lako lijifunze kuangalia mazuri badala ya mabaya. Wote tulizaliwa tukiwa safi, Mwenyezi Mungu anatupenda sisi sote na mabaya yetu, upendo wake hauna mipaka, anataka sisi tubadilike na tuwe na upendo kama yeye. Mpendwa msomaji, kuna mtu unamchukia, usiendelee kumchukia, kuendelea kumchukia ni kama mtu ambaye yupo kwenye giza umpeleke kwenye giza zito zaidi, mwoneshe upendo jinsi ulivo na hiyo ndiyo nuru ambayo anatakiwa kuipata mtu ambaye yupo kwenye giza.
2. Sababu ya pili ni ubinafsi. Mpendwa msomaji, ubinafsi ni kitu kibaya sana, ubinafsi unapelekea magomvi kwa watu. Ubinafsi ni hali kujiona wewe unastahili kulingo wengine. Ubinafsi ni kitu kibaya sana, ubinafsi unapelekea kuwa na maisha magumu sana. Mpendwa msomaji, unapokuwa mbinafsi unashindwa kuona thamani ya wengine, kila kitu ambacho unafanyiwa utaona hakifai kwako. Tabia hii si nzuri na itakutesa sana mwenyewe lazima utambue thamani ya wengine na kuwajali.
Upendo ndio hali pekee ambayo imeshinda haya yote. Ukweli ni jambo ambalo litaondoa hofu na maumivi. Ishi kweli na upendo, maisha yako yatakuwa mazuri.
Endelea kutembelea blogu hii kujifunza zaidi.
Wako Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment