Ukichukua andazi na kumpa mwingine yale mafutafuta na harufu nzuri ndicho kitu ambacho unahitaji. Huu ni ukweli na ndio uhalisi wenyewe.
Ukijenga nyumba kubwa, siyo nyumba hiyo ndiyo ulikuwa unahitaji. Ni sehemu ndogo tu, ambayo unaweka kitanda na si sehemu yote ya kitanda utalalia bali sehemu. Huu ndio ukweli na ndio uhalisi wenyewe.
Si chakula chote ambacho unakula ndicho unahitaji, bali ni sehemu ndogo sana ambayo hufyozwa kama mafuta ya maandazi ambayo hubaki mkononi, ambacho baadae kufanya, damu. Huu ndio ukweli halisi ambao hauwezi kupingwa.
Si kila kitu ambacho unasima ni kinakufaa, bali ni sehemu ndogo sana ambayo katika kitabu utaikumbuka. Huu ndio ukweli halisi na hauwezi kupingika.
Siyo maneno ninayoandika ndiyo unahitaji, bali ukielewa hutahitaji tena maneno yangu. Huu ndio ukweli halisi na hauwezi kupingika.
Je! Ni kitu gani ambacho unahitaji? Ni kitu gani kilicho chako?
Ni kile ambacho huna ndicho chako. Kile ambacho hujashika ndicho chako.
Chochote ambacho unacho siyo chako. Chochote ambacho umeshika na kumiliki si chako.
Aliyenacho huwa anagawa na asiye nacho huwa anapokea.
Usifikiri kijinga, kuwa kile ambacho huna ndicho huna. Lakini pia usifikiri kijinga kwamba kile ambacho unacho ndicho chako.
Tunachohitaji sisi ni uhai. Vyote vinavyopita katika mikono yetu vinatuachia alama. Mapito ya maisha yetu yametuachia alama. Alama ndio zawadi yetu.
Tunaishi sasa kwa utambuzi kwa utambuzi, utambuzi unaotokana na makovu ya hapo nyuma. Haijarishi tulipitia katika mabaya ama mazuri, yote yaliacha kovu, kama mafuta na harufu ya andazi inayobaki katika mikono yako.
Mpendwa msomaji, kama bado mpaka leo huishi maisha ya furaha na umebahatika kusoma makala hii fupi, basi, leo hii nenda nyumbani, kajifungie mlango, peke yako, kafanye sala ya shukrani, kamshukuru Mungu kwa mapito uliyopitia na yakakuachia kovu la kumbukumbu. Mchukuru Mungu kwa kila kitu, haijarishi mapito yako yalikuwaje, mabaya ama mazuri. Lakini kwa sababu leo unatambua tifauti, hiyo ndiyo zawadi yako.
Ona wema kwenye kila jambo.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment