JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • ushauri
    • KUHUSU SISI
    • MAISHA NDANI YA YESU
  • MAWASILIANO
    • NAMBA YA SIMU
      • Sub 0687000768
      • Sub Child Category 2
      • facebook
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • NJOZI
  • SAIDIA HUDUMA HII
    • Childcare
    • Doctors
  • NYUMBANI
  • KUFURAHIA MAISHA
    • Stock
  • TAFAKARI YA ROHO
    • HEKIMA ZA WAZEE
    • Games
    • AFYA
      • Office
  • MAHUSIANO
    • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • USHAURI
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
    • Childcare
    • Doctors
  • PATA BLOGU

Thursday, October 4, 2018

Hata Kama Umezaliwa Kwa Injili Ya Maji Na Roho Unahitaji Kujitakasa Kwa Maombi.

 Sadick Kilasi     October 04, 2018     KUFURAHIA MAISHA, TAFAKARI NENO YA SIKU     No comments   

Wakati Yesu alipokuwa tayari amekamirisha tendo la kuchukua dhambi katika mto Yordani, alipobatizwa Yohana alifunza wanafunzi wake tendo la kujitakasa ili waendelee kufurahia katika upo wa Mungu.

Mathayo 13:3-10, Yesu, hali akijua Baba amampa vyote mikoknoni mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile ktambaa alichojifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simoni Petro, Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, wewe hujui sasa, lakini utalifahamu baadae. Petro akamwambia, wewe hutanitawadha miguu kamwe , Yesu akamwambia, Kma usipotawadha huna shirika nami. Simani Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia. Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi lakini si nyote.

Ikiwa umezaliwa upya kwa kuamini injili ya maji na Roho basi unahitaji kujitawadha wakati wote na hii inatokana na mazingira ambayo unaishi kwa sababu kuna mengi hutukia kwahiyo unahitaji kujiweka safi. Hii ni tifauti na kuomba toba, ni tofauti kabisa na ndiomaana Yesu anasema, mnahitaji, kujitawadha miguu yenu kwani mmekuwa safi tayari. Unapaswa kuingia katika maombi na kuombea yale machafu yaliyokuingia katika dhamiri yako. Ili kwa yule ambaye hajazaliwa kabisa katika injili ya maji na Roho, hawezi kujitawadha kama huyu aliyezaliwa upya tayari. Huyu anapaswa kuomba toba, toba ambayo ndiyo mwanzo wa kugeuka na kuiamini injili ya Maji na Roho. Hata kama unamwamini Yesu ila kama hujazaliwa katika injili ya maji na Roho, unapaswa kuifahamu injli hii ili kuzaliwa upya. Na ndio maana Yesu alisema sio wote ambao wametakaswa bali kunawengine bado hawajatakaswa.

    KUINGI KWA UCHAFU HATA KAMA UMEZALIWA MARA YA PILI.
Hakuna kitu ambacho kipo katika Agano la Kale na kimekosekana katika Agano jipya, mambo yote yanafanana. Agano jipya ni ufunuo wa Agano la Kale. Hata injili ya maji na Roho, kwenye Agano la Kale ipo, na ndio hiyo hiyo ambayo inachukua dhambi zetu kwa sasa. Sasa katika kuombea na kujitakasa, Agano la Kale limefafanua jambo hili namna machafu huingia katika dhamiri zetu.

 1Wafalme  22:29-34,Basi Mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda  wakakwea mpaka Ramoth-Giliadi. Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, nitajibadilisha na kuingia vitani; lakini wewe uvae mavazi yako. Mfalme wa Israeli akajibadilisha, akaingia vitani. Basi Mfalme wa Shamu  alikuwa amewaamuru wakuu wa magari yake thelathini na wawili, akisema msipigane na mdogo wala mkuu, ila na Mfalme wa Israeli peke yake. Ikiwa wakuu wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, huyu ndiye Mfalme wa Israeli. Wakageuka juu yake ili wapigane naye; naye Yehoshafati akapiga ukelele. Ikiwa wakuu wa magari walipoona ya kuwa siye Mfalme wa Israeli, wakageuka nyuma wasimfuate. Mtu mmoja akavuta upinde wa kubahatisha, akampiga Mfalme wa Israeli mahali pa kuungana mavazi yake ya chuma; kwa hyo akamwambia mwendesha gari lake , geuza mkono wako, unichukue kutoka katika majeshi; kwa kuwa nimejeruhiwa sana.

Basi ni vizuli kuvaa silaha za kiroho wakati wote, usifanye maamuzi  bila kumshirikisha Mungu. Shetani anachotaka yeye ni kuondoa furaha yako, basi, na furaha yetu ni uwepo wa Mungu ndani yetu si kwa kujitegemea sisi wenyewe. Adui huangalia fursa kwako wakati wote, anaangalia upenyo kwa kukupiga mshale, wakati wote ni vita.

Ukijikuta unapoteza kwa sababu ya mshale wa Adui jambo la kwanza ni kumwangalia Yesu na kuomba akutakase. Yeye kwa sasa amefanyika kuwa kuhani wetu mkuu, ameketi mkono wa kuume akiendelea kututakasa.

Waebrania 8:1-4, Basi, katika hayo tunyosema, neno lililo kuu ndilo hili, Tunaye kuhani mkuu namna hii, aliyeketi mkono wa kuume  wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliweka na si mwanadamu. Maana kila kuhani mkuu huweka ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa. Kma angalikuwa juu ya nchi asingalikuwa kuhani; maana wapo watoao sadaka kama iagizavyo sheria;

Mtu yeyote yule ambaye amezaliwa Upya amefanyika kuhani wa duniani, anapaswa kuhubiri injili, kwani ndiyo kazi ambayo Mungu aliagiza, lakini ukuhani wa mtu aliyezaliwa upya duniani ni kivuli cha kuhani mkuu wa mbinguni katika kiti cha enzi, yeye ndiye kuhani wetu mkuu wa watakatifu. Watu wote ambao wamezaliwa upya kuhani wao ndiye Yesu, ambaye ndiye kuhani wa mbnguni.

Hesabu 21:7-9, Watu wakamwendea Musa, wakasema, tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; tumbee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. Bwana akamwambia Musa, jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akaifanya nyoka ya shaba akaiweka juu ya mti mti, hata ikawa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Yesu ndiye kwa sasa tunamtazama kama vile wana wa Israeli walivyomtazama nyoka wa shaba. Ikiwatayari umempoea Roho MTAKATIFU, unapaswa kuishi maisha mapya na siyo kunung'unika kama wana wa Israeli lakini ikiwa tayari nyoka amekugonga basi wapaswa kuishi kwa kumwangalia Yesu. Kama vile wana wa Israeli walivyomtaama nyoka.

Yohana 19:31-37, Basi Wayahudi kwa sababu ya maandalio ya , miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, [maana sabato ile ilikuwa siku kubwa], walimwomba pilato miguu yao ivunjwe ikaondolewe. Basi askari wakaenda wakaivunja miguu wa kwanza na wa pili, aliyesurubiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua kwa kuwa anasema kweli ili nanyi mpate kusadiki. Kwa maana hayo yalitimia ili andiko litimie, hapana mfupa wake utakaovunjwa.. Na tena andiko lingine lanena, watamtazama yeye waliyemchoma.


Yesu ndiye tumaini kwa wote, ambao hawajazaliwa upya ni lazima wamtwishe dhambi Yesu, kwa kuamini injili ya maji na Roho, ambayo lazima uamini katika maji, damu na Roho. Maji ni katika ubatizo wake, ambao ndio ulimtwisha dhambi Yesu, damu ni mateso yake msalabani, ambapo alifanya agano la upatanisho na kuteswa kwa sababu ya dhambi alizotwishwa alipobatizwa na Yohana Mbatizaji, katika mto Yordani na Roho ni Uungu wake, kwamba Yesu alifufuka kwa sababu ya uweza wa Roho ya Mungu. Kwa yule ambaye hajazaliwa upya anapaswa kuamini hivi. Akitubu kwa kukiri kwamba yeye alizaliwa katika dhambi kiasili na yeye mwenyewe hutenda dhambi na mshahara wake ni mauti, kwenda motoni basi toba yake ni kugeuka na kumwamini Yesu, na unamwamini Yesu kwa kushriki hatua hizo tatu.

1Yohana 5:4-7, Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda Ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mwenye kushinda Ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Hii ndiyo injili ambayo huwaponya wale ambao hawajazaliwa upya kabisa, wanapaswa kuamini hivi.

Wale ambao wamezaliwa upya wanapaswa kuvaa siraha za kiroho wakati wote, wao ni makuhani wa duniani ambao huwapatanisha watu na Yesu lakini nao pia wanaye kuhani mkuu ambaye ndiye Yesu, kwani hapa duniani watu wote tupo safarini hatuna makao. Kila kitu huwa kina hatua zake yaani ngazi, mtu ambaye hajazaliwa upya anamtegemea yule aliyezaliwa upya ampatanishe na Yesu kwa kumhubiria injili ya kweli, kwani watu wengi bado wapo gizani katika hili. Lakini na yule aliyezaliwa upya anamtegemea Yesu ampatanishe na Mungu. Walio zaliwa upya kwa kuamini injili ya maji na Roho ambayo YESU mwenyewe alihubiri, wana wito wa kuhubiri injili lhapa duniani lakini nao matumaini yako makubwa ni kuufikia utukufu wa Mungu kikamirifu, kuvishwa mwili mpya, humtegemea YESU azidi kuwaelekeza juu ya patakatifu pa mbinguni.

Injili hii haitegemei kwenda kubatizwa katika maji mengi ama machache inakutegea wewe uamini tu, ikisha ukisha kuamini ufanye mapenzi ya Mungu. Asikudanganye mtu eti kwamba nimebatizwa katika maji mengi ama machache, hapana, inategemea imani yako. Ni lazima umtwishe dhambi Yesu, siyo wewe kubatizwa, Mapenzi ya Mungu sisi wanadamu tumtwishe dhambi Yesu, ili sisi tuwe huru na tunamtisha pale alipoamini hatua alizopitia. Ubatizo wa kubatizwa kwa maji na mtu, mengi au machache ni matendo ya nje ambayo huonyesha upo pamoja na wengine. Lakini ukweli halisi upo ndani. Ubatizo wa tohara ya moyo sio kuondoa matendo ya nje bali moyoni mwetu na dhamiri zetu.

1Petro 3:21, Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi siku hizi; [siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu], kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.

Yeyote ambaye amezaliwa upya hana dhambi ndani ya moyo wake. Tohara imefanyika ndani ya moyo wake. Kma ilivyokuwa dusturi katika Agano la Kale;
Kutoka 12:48, Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kumpenda kumfanyia Bwana pasaka, waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa  mfano mmoja wa mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu yeyote aliyetahiriwa asimle. Tohara hii ilikuwa ni ya kuondoa govi la mbele lakini ilikuwa haiondoi dhambi moyoni bali ilikuwa mfano tu.

Unaweza kujiuliza mbona sasa tohara huwahusu wanaume? Ukweli ni kwamba Mungu anapowahesabu watu, mwanamke huhesabiwa kwa upande wa mwanamme kwani alitoka kwenye ubavuwa mwanaume.

Unapaswa kuamini injili hii na kupokea wokovu wa Mungu. Kuijua zaidi injili hii unapaswa kusoma zaidi kitabu cha UKRISTO NA MAISHA, kitabu cha bure kabisa. Nitumie ujumbe nikutumie kitabu Whatsap.  Asante.

Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.

Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
  • Share This:  
  •  Facebook
  •  Twitter
  •  Google+
  •  Stumble
  •  Digg
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

Translate

Total Pageviews

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile

Followers

Kurasa

  • Nyumbani
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

Search This Blog

Blog Archive

  • ►  2020 (5)
    • ►  January (5)
  • ►  2019 (46)
    • ►  December (4)
    • ►  October (1)
    • ►  July (8)
    • ►  June (1)
    • ►  May (2)
    • ►  March (14)
    • ►  February (11)
    • ►  January (5)
  • ▼  2018 (275)
    • ►  December (17)
    • ►  November (25)
    • ▼  October (29)
      • Maisha Yenye Maana.
      • Wapi Ulipo?
      • Sala Ya Kuomba Amani.
      • Sicho Hicho Ndugu Yangu Unachohitaji.
      • Mwili Wako Ni Zawadi Kwa Wengine.
      • Utabiri Unaonesha Kwamba Wewe Utafurahia Maisha Ka...
      • Unachohitaji Katika Maisha Yako.
      • Kutambua Dalili Za Kujiliwa Kwa Jambo Jipya.
      • Ishi Kwa Kudhamiria Jambo Jema.
      • Ubatizo Ni Nini?
      • Upekee Unagharama Yake Ya Kulipa.
      • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache,...
      • Uogope Woga unaokufanya Uwe Mwoga.
      • Jifunze Kwa Bidii Ili Uwe Huru.
      • Wakati Jama Wakati.
      • Madamu Unayo Leo Unaweza.
      • Viungo Vya Mwili Hufanya Kazi Kwa Ushilikiano.
      • Dunia Mama Haimtupi Mwenye Mwili.
      • Mwalimu Nyerere Zawadi Ya Afrika Na Dunia Kwa Ujumla.
      • Mambo Ya Kujua Na Kuepuka Ili Kudumisha Furaha Kat...
      • Unabadilisha Nguo Kila Siku, Kwanini Usibadilishe ...
      • Angalia Mbegu Unazokazana Kupanda.
      • Usikazane Kutafuta Raha Katika Maisha Bali Kazana ...
      • Ujumbe Uliobeba Ndani Yako.
      • Kila Mtu Yupo Bize Na Lugha Yake.
      • Mambo Ya Kuyatambua Katika Maisha Lakini Kuzingati...
      • Mwenyezi Mungu Ni Nani?
      • Hata Kama Umezaliwa Kwa Injili Ya Maji Na Roho Una...
      • Tujifunze Kutoka Kwa Panya Na Kuishi Maisha Yenye...
    • ►  September (43)
    • ►  August (7)
    • ►  July (12)
    • ►  June (17)
    • ►  May (19)
    • ►  April (31)
    • ►  March (33)
    • ►  February (25)
    • ►  January (17)
  • ►  2017 (58)
    • ►  December (16)
    • ►  November (22)
    • ►  October (2)
    • ►  September (11)
    • ►  August (4)
    • ►  July (3)
Sadick Kilasi. Powered by Blogger.

Jisajili kwa kujiunga nasi hapa

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
Maisha yenye maana ni yale maisha ambayo mhusika atambua nini kusudi lake la kuwepo hapa duniani. Hapandipo muhusika anapo kaa katika nafasi yake na kuwasha nuru katika sehemu aliopo kutokana uhusika wake. Jiunge na mtandao huu kupata maarifa zaidi na kwa ushirikiano mwingine kwa ujumla.

Kurasa

  • Nyumbani
  • TAFAKARI ROHO
  • Saidia Huduma Hii Kuwafikia Wengi Zaidi.

JIUNGE NASI SASA KWA KUJAZA FOMU HAPO CHINI


ANZA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA YESU, MPOKEE ROHO MTAKATIFU KWA INJILI YA MAJI NA DAMU 0687000768

Zilizosomwa sana

  • Chukua hizi hapa nukuu za Malcolm x mtu ambaye anawavutia wengi sana.
    Ni siku nyingine tena ambayo ni mpya kabisa, karibu tena katika blogu hii ya JIKO LA USHAURI ambapo mimi mpendwa wako nimekuwa naingia jikon...
  • Ubatizo Wa Maji Mengi Na Ubatizo Wa Maji Machache, Upi Ni Sahihi?
    Ubatizo wa Maji Mengi Na Maji Machache. Kumekuwa na migongano kwa muda mrefu sana juu ya ubatizo, kati ya ubatizo wa maji mengi na ule uba...
  • Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa.
    Falsafa Za Maisha, Yaani Neno La Maarifa. Habari mpendwa? Natumai wewe unayesoma hapa umzima.   Karibu tena katika Falsafa Za Maisha. Ku...

Blog Archive

  • July 2017 (3)
  • August 2017 (4)
  • September 2017 (11)
  • October 2017 (2)
  • November 2017 (22)
  • December 2017 (16)
  • January 2018 (17)
  • February 2018 (25)
  • March 2018 (33)
  • April 2018 (31)
  • May 2018 (19)
  • June 2018 (17)
  • July 2018 (12)
  • August 2018 (7)
  • September 2018 (43)
  • October 2018 (29)
  • November 2018 (25)
  • December 2018 (17)
  • January 2019 (5)
  • February 2019 (11)
  • March 2019 (14)
  • May 2019 (2)
  • June 2019 (1)
  • July 2019 (8)
  • October 2019 (1)
  • December 2019 (4)
  • January 2020 (5)

JIKO LA USHAURI

Itambue Injili Ya Maji Na Roho. Ushiriki Ufalme wa Mungu, pata kitabu cha bure. Wasiliana nasi kwa sadikila65@gmail.com.

Tags

  • BIASHARA
  • HEKIMA ZA WAZEE
  • KUFURAHIA MAISHA
  • KUPATA BLOGU
  • MAHUSIANO
  • MAWASILIANO
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI
  • NJOZI
  • PATA BLOGU
  • SAIDIA HUDUMA HII
  • TAFAKARI NENO YA SIKU
  • TAFAKARI YA ROHO
  • UJASIRIAMALI
  • USHAURI
  • USWAZI TRICK

Kurasa

Labels

  • HEKIMA ZA WAZEE (24)
  • KUFURAHIA MAISHA (76)
  • KUPATA BLOGU (2)
  • MAHUSIANO (81)
  • MAWASILIANO (1)
  • NENO KUTOKA KWA SADICK KILASI (8)
  • NJOZI (94)
  • PATA BLOGU (3)
  • TAFAKARI YA ROHO (57)
  • UJASIRIAMALI (31)
  • USHAURI (78)
  • USWAZI TRICK (9)

Loading...

Fomu ya Anwani

Name

Email *

Message *

  • Napenda kusoma Biblia

About Me

Sadick Kilasi
View my complete profile
INJILI YA MAJI NA DAMU.

Search This Blog

Chapisho Lililoangaziwa

Alipambania Tumaini Lake Na Ndoto Yake Ikawa Kweli.

Kila mtu katika maisha ana tumaini lake. Msingi mkuu wa maisha ni tumaini. Nguvu kubwa ya maisha ni imani na mapito makuu ya maisha ni u...

Posts
Atom
Posts
Comments
Atom
Comments
INJILI YA KWELI NI INJILI YA MAJI NA ROHO. (MAJI, DAMU NA ROHO).
HII NDIYO KWELI YENYEWE.
YOHANA 19:34-35.

Copyright © JIKO LA USHAURI | Powered by Blogger
Design by Hardeep Asrani | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com | Distributed By Gooyaabi Templates