Tumaini lenye mwelekeo chanya ndicho kitu ambacho kila mmoja mwenye mwili anahitaji kuwa nacho. Kila kiumbe hufikiri kuendelea mbele na kuiandaa baadae kwa imani.
Kwa wenye imani na Mungu hutumaini kupokea haki ya Mungu huku tumaini lao la
mwisho ni kuingia katika paradiso. Imani ni kuvuta tumaini la baadae na kuishi sasa.
Watu wengi hawana furaha katika maisha yao kwa sababu meli yao haina sehemu ya kutia nanga. Meli yao yaani maisha yao hubaki kuzurura huku na huko huku wakiwa hawana tumaini lolote. Imani ni kuwa na hakikika na mambo yatarajiwayo yasiyoonekana kwa macho. Uhakika wa mambo ya baadae ndio hufanya kila kiumbe kile chakula, kukua na mengineyo.
Kama mtu amekosa tumaini na imani, basi, amekosa maana ya maisha na hana maisha, amekufa kwa lugha nyingine. Kwa sababu kifo huwatawala watu walio hai na sio waliokufa.
Tunachohitaji sasa ni tumaini lenye mwelekeo chanya, na tuishi sasa kwa imani. Kilicho muhimu sasa imani ya kuishi matumaini. Hakuna kitu chenye thamani kubwa kama sasa, maamuzi ambayo utachukua sasa ndiyo yatafanya ulifikile lile tumaini lako kuu. Haijarishi ni tajiri ama maskini ni lazima kuwa na matumaini. Wote wenye mwili wanaishi matumaini kwa imani. Matarajio madogo madogo ambayo huyafikilia na kufanya haya ndiyo hutupeleka Mwenye tumaini kuu mwisho.
Usiishi kama mfungwa wa mtazamo hasi, bali ishi kama mfungwa wa matumaini. Usijihesabie haki mwenyewe bali jiweke chini ya uwepo wa Mungu ambaye kwa yeye utapokea haki ya imani na kukufanya uendelee kusonga mbele. Mungu alimeambia Abraham, mimi ni Ngao yako na tuzo lako. Ikiwa Mungu yeye aliyeumba mbingu na nchi amekupa leo ahadi hii ni wazi kwamba utakuwa na furaha ya kutosha na utaishi kwa imani. Na ndivyo ilivyo hata sasa, sisi tunaishi kwa imani, imani ambayo Kristo Yesu ameanzisha. Wakati huo Abramu alikuwa ni mzee lakini bado aliamini kwamba Mungu atatimiza ahadi yake. Mungu alimwambua toka nje angalia juu, nitakujalia watoto kama nyota juu angani.
Mungu yule yule ambaye alimwahidi Abramu ndiye hata sasa, sisi tunayemtumainia kwa imani kwa njia ya Kristo Yesu, anatuambia tumutumainie yeye. Katika Zaburi ya ishirini na saba, anatuambia kwamba tutumainie kwake. Lakini katika kutoka anatuambia kwamba tusimame imara naye atatupigania. Je! Wewe umewekeza wapi tumaini lako? Meli yako imetia wapi nanga?
Kitu pekee ambacho unapaswa kuwa nacho ni kumtumainia Mwenyezi Mungu na kuishi kanuni za Mungu kwa imani. Zipokee ahadi zake kwa imani. Timiza mapenzi yake kwa imani.
Haijarishi wewe unaona kana kwamba bado, ama imani yako ndogo, hapana, kwa kadili ambavyo unawekeza imani yako kwa Mungu, ndivyo unazidi kupokea haki yake. Kwa kadili ambavyo unavaa utayari wa kusoma neno la Mungu ndivyo imani yako inakua.
Ni bora kumtumainia Mwenyezi Mungu, na kuishi maisha ya furaha kuliko kukosa tumaini na kuishi maisha ya hovyo ya kuandamwa na kifo hapa hapa duniani.
Mtumainie Mwenyezi Mungu, uwe na moyo, usikate tamaa, naam, mtumainie Mwenyezi Mungu.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment