Kosa kubwa ambalo watu wengi tumekuwa tunafanya ni kuishi bila kudhamiria. Watu wengi tumekuwa tunaishi maisha yale ya amka twende. Mtu mmoja alishawahi kusema, watu wengi wanaamka kimwili na sio kiakili.
Hili ndilo kosa kubwa wengi tumekuwa tukifanya. Wengi wetu tumekuwa tukiamka na kukurupuka tu bila kujali nini kinaendelea katika maisha yetu. Maisha haya mara nyingi yamekuwa yakikosa ubora kwa sababu ni rahisi kwa mtu kuharibiwa siku na mwingine kwa sababu hakuna kitu mtu amedhamiria kuindesha siku yake.
Mtu mmoja alisema, usipo simama na chochote, utadondoka na chochote.
Dhamiria kufanya jambo linalofaa kabla ya kufanya, dhamiria kusamehe kabla ya kukosewa, dhamiria wema kwenye kila jambo.
Yesu alisema, ikiwa mtu ametokwa na pepo, harafu, pepo ikaenda jangwani kutangatanga na sehemu za maji, hujisemea, nitarudi nyumbani kwangu, akisha kurudi na kuona nyumba imefagiliwa vizuri, huenda kuwaita pepo wengine saba walio wabaya zaidi, na mtu atakuwa na hali mbaya zaidi ya mwanzo.
Rafiki, ubongo wako isiwe sehemu ya pepo wachafu kuishi. Dhamiria kufanya mazuri, dhamiria kifanya makubwa. Njia rahisi ya kuishi maisha yenye maana ni kudhamiria.
Dhamiria kumsaidia mwingine, dhamiria kufanya kitu kikubwa. Katika kitabu cha Zaburi, neno linasema, wokovu wake u karibu na wamchao, utukufu ukae katika nchi yetu. Maisha so bahati, maisha ni ukweli.
Utapata haki endapo upi jilani na haki, chakula kitaingia mdomoni endapo umefungua mdomo. Utasamehe endapo ulidhamiria kusamehe.
Usitegemee bahati katika kuishi, bali dhamiria kila kitu. Joyce Meyer anasema, tarajia mambo mazuri yatokee. Ishi kwa kudhamiria kuishi ili usiendeshwe na kuishi.
Ishi kwa kudhamiria kwenye kila kitu.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65@gmail.com.
0 comments:
Post a Comment