Tunaishi katika dunia ya wenye mwili, tumetoka katika hali ya kutokuwa na mwili yaani katika Ulimwengu wa Roho. Tulikuwepo kabla ya kuwepo, tumepewa mwili ili kuonekana kwa wengine kama zawadi yao.
Waebrania 10:5-7, Kwahiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo ulisema, tazama, nimekuja, [katika gombo la chuo nimeandikiwa] niyafanye mapenzi yako.
Kristo Yesu alikuja kama zawadi ya ulimwengu, alikuja kama mwanadamu wa kawaida ili kwa yeye dhambi ya ulimwengu ichukuliwe katika mwili wake. Lakini pia Yesu aliacha ukumbusho wa nano lake. Leo hii ulimwengu unasafishwa na kufanywa upya kupitia yeye. Yesu alikuja kwa ajli ya ulimwengu, na kama Yesu alikuja kwaajili ya ulimwengu basi ni wazi kwamba aliacha mfano ambao kila mwenye mwili anapaswa kuufuata.
Kama umekuwa unajihesabia haki kupitia mwili wako ni wazi kwamba unajikosea wewe mwenyewe. Wewe ni zawadi kwa wengine, wewe ni kwaajili wengine. Kazana kutoa thamani kwa wengine ili kutimiza lengo ambalo Mungu alitaka utimize.
Haijarishi upo katika hali gani? Bali kuna upekee ambao Mungu alitaka uwasilishe katika ulimwengu. Usiangalie ni kitu gani huna, bali angalia ni kitu gani unacho na ukifanye kikue. Usiangalie watu wanafanya nini bali angalia namna ambavyo unaweza kuupa ulimwengu kile ulichhonacho. Ikiwa kama utaangalia kile ambacho huna huwezi kujikubali, ikiwa itaiga vile ambavyo wengine wanavyo, basi, mwili wako hauna maana kuwepo duniani.
1Wakorintho 14:7, Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, ikiwa ni vilimbi, ikiwa ni kinubi, visipotoa sauti zilizo na utofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi?
Angalia ni namna gani na sehemu gani ambayo ulimwengu unapaswa kulishwa na wewe. Ikiwa unafanya vitu ambavyo wanafanya wengine, itakuwa ni makelele sasa. Hata kama wengine hufanya jambo zuri kiasi gani? Lazima utambue kwamba hata wewe unauzuri wa kipekee. Simaanishi labda usifanye kizuri cha mwingine, hapana, bali tambua chako cha kipekee kiwe shina lako. Hata mti huwa unashina ambalo hubeba matawi makubwa na madogo.
Tumezaliwa tofauti, tuna sura tofauti, tuna sauti tofauti, na hii ndio zawadi kubwa ya ulimwengu, huo upekee wako. Ikiwa unakitu kizuri ndani yako si chako, hicho ni kwaaajili ya wengine.
Waebrania 13:10, Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake.
Je mtu anaweza kujidaia kipawa chake yeye mwenyewe bila kudhihirisha kipawa hicho kwa wengine? Lazima kuwepo na wengine wanaopenda kipawa chako. Kila unachofunua nje ya ulimwengu hicho si chako.
Kazana utoe thamani kwa wengine uwape watu zawadi hiyo. Kilicho chako ni kile ambacho huna.
Sadick Kilasi wa jikolaushauri.blogspot.com.
Mawasiliano ni 0687000768 au sadikila65gmail.com.
0 comments:
Post a Comment